Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mtikila atakwenda jela endapo atashindwa kulipa deni


Monday, March 08, 2010 10:58 AM
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, imeamuru kunadiwa kwa mali za Mchungaji Mtikila ili kuweza kulipa deni linalomkabili kinyume na hapo atakwnda jela.
Uamuzi huo wa Mahakama umekuja baada ya ombi la kumtaka mchungaji kufungwa jela baada ya kushindwa kulipa deni la silingi milioni 8 analodaiwa.

Hivyo mahakama imeamuru kudainiwa kwa mali zake ili kuweza kufidia kulipa deni hilo na endapo itashindikana ombi la kufungwa kwake litazingatiwa.

Awali Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliamua nyumba ya mchungaji huyo iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam iuzwe ili kufidia deni hilo, lakini Hakimu Hakimu Afumwisye Kibona alisitisha uamuzi huo na kuagiza mali zake nyingine ziuzwe kufanikisha malipo ya deni hilo.

Mtikila na mwenzake Mariam Issa wanadaiwa zaidi ya Shilingi milioni 8 na Pascazia Matete ambaye alidai aliwakopesha kwa ajili ya kufanyia biashara.

Matete alishinda kesi namba 78 ya mwaka 2008 aliyoifungua katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo mbele ya Hakimu Benjamin Mwakasonda.

Akitoa amri hiyo, Hakimu Kibona alisisitiza kuwa iwapo ombi hilo la kutafuta mali mbadala za Mtikila ziuzwe kwa ajili ya kulipa deni hilo halitafanikiwa, ombi la kumfunga jela litafuatia.

Uamuzi huo wa kumfunga au kutomfunga utatolewa Machi 18, mwaka huu na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde.

Awali baada ya Matete kushinda kesi hiyo kutokana na Mtikila kutohudhuria Mahakamani mara kwa mara, aliiomba mahakama iamuru nyumba ya Mtikila yenye namba MKC/MCB 1135 iliyo kwenye kiwanja namba 237, Kitalu C Mikocheni iuzwe ili alipwe deni lake.

Hata hivyo, ombi la kuuza nyumba hiyo lilishindikana baada ya kampuni ya kimataifa ya Cielmac kuwasilisha pingamizi ikieleza kuwa ilishanunua nyumba hiyo kwenye mnada uliofanywa na benki ya NBC kupitia kampuni ya Comrade Auction Mart $ Court Brokes baada ya Mtikila kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15 milioni aliouchukua katika benki hiyo.







 
Na Pilly Kigome, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: moud     Monday, March 08, 2010 12:18:18   
 
dhuuuuuuuu huyu mchungaji nitapeli kweli .
 
 
Mtoa Maoni: MINA    Monday, March 08, 2010 12:35:23   
 
ha ha ha ha mae naomba nisiongee chochote yani ungekuwa BABA yangu ingebidi nikuachie laana mana we mzee CHIBOKO
 
 
Mtoa Maoni: Semenya    Monday, March 08, 2010 13:13:21   
 
Hahaaaaaa MINA unavyetua na wewe maskini kizere cha Mungu!
 
 
Mtoa Maoni: dafson    Monday, March 08, 2010 16:02:13   
 
minaona hata jina la uchungaji ulifute kabisa.
 
 
Mtoa Maoni: KAMILA USA    Monday, March 08, 2010 17:22:46   
 
MiNa na SeMeNya, naona hapa mpo mia kwa mia.
Eti huyu baba CHIBOKO, no ni KIVOKO ya maneno

 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Polisi kwa kete 300 za bangi
> Tani za mtama usiofaa wakamatwa Zanzibar
> Jeshi la Polisi laimarisha ulinzi Kariakoo
> Tendwa atupilia mbali pingamizi la Chadema
> Aangua kilio baada ya kutapeliwa- Kar iakoo
> Sheria isipofata mkondo wake, nitaandaa maandamano-Baswalehe
> Darasa la 7 waanza mitihani leo
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Chadema yawasilisha pingamizi
> Wanafunzi waweweseka Tabata
> Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma yateketea
> Ramli ya Joseph ilisema hivi!
> 7 papohapo, wengine majeruhi ajalini- Mabibo
> Makahaba msipotoshe vazi hili!
> Sakata la kugombania maiti bado tata
> Mahakamani kwa kujipatia ngono kwa njia ya madawa ya kulevya
> Chadema yamuwekea pingamizi Kikwete

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
9 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake