Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Serikali yaamuru umeme upitishwe Kanisa la Kakobe


Monday, March 08, 2010 10:38 AM
HATIMAYE Serikali imeamua kupitisha waya za umeme wa msongo wa kilovolti 132 karibu na Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Serikali imetoa amri hiyo bila kupingwa baada ya kuridhika na taarifa iliyotolewa na kitengo cha utoaji ushauri cha Chuo Kikuu (BICO).

Jana Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja,akizungumza na waandishi wa habari alisema utekelezaji wa mradi huo unatakiwa kufanyika mara moja kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi, kwani ni kwa ajili ya manufaa na ustawi wa taifa.

Alisema serikali imechukua hatua hiyo baada ya kuridhika na utafiti uliofanywa na wataalamu washauri wa BICO, TANESCO na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) umehakikishia serikali kuwa umeme huo hauna madhara kwa wananchi.

“Hivyo TANESCO inatakiwa kuendelea na zoezi la upitishaji wa nguzo za umeme katika eneo hilo” alisema Waziri.
Awali alisema kuwa kuna taarifa zilidai kuwa vipimo vya kupitihsa umeme huio kanisani hapo vilikosewa lakini iliundwa tume kuthibitisha hilo.

Hata hivyo alisema baada ya uchunguzi ilibaini hakuna vipimo vilivyokosewa na maamuzi yalithibitishwa na pande zote mbili kuthibitisha hilo.

Hivyo baada ya kuafikiana na uamuzi huo, Kakobe aliiomba serikali kufikiria kubadilisha laini na kuziweka katikati ya barabara ya Sam Nujoma kwa kuwa bado anaamini kuwepo kwa madhara ya mitambo yake ya televisheni.

Hata hivyo, Waziri Ngeleja alisema serikali haitaweza kupitisha laini hiyo katikati ya badabara, kwani sehemu hiyo kumesimikwa taa za barabarani na pia inakusudiwa kutumika kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kasi.

Aliongeza kuwa serikali haiwezi kubadili usanifu wa mradi huo kwa vile hakuna uhakika endapo maombi hayo ya kujenga kituo cha televisheni yatakidhi vigezo vyote ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masafa.

“Kwa kweli serikali haiwezi kufanya kazi kwa kuhisi, kwani TCRA imethibitisha haijawahi kupokea wala kufanya mchakato wa maombi kutoka kwa kanisa hilo,” alisema Ngeleja.

Alisema BICO katika taarifa yake imeitaka TANESCO kutumia mbinu bora za ujenzi wa laini ya msongo huo, ili kuepukana na kona kali kwenye waya na kutounganisha waya sehemu yoyote kati ya nguzo namba 18 na 19 ambazo ziko kwenye eneo la karibu na kanisa hilo.

Katika taarifa hiyo ya Waziri iliongeza kuwa serikali imetumia shilingi milioni 25 kwa ajili ya kumlipa mshauri mtaalam BICO hadi kukamilika kwa ripoti hiyo ambayo imeweza kuondoa utata uliokuwepo kuhusiana na madai ya kuwepo kwa madhara.

Alisema mradi huo utahakikishwa unamalizika haraka iwezekana kwa kuwa kwa kiasi kikubwa utapunguza kukatika katika kwa umeme kunakosababishwa na uhaba pamoja na uchakavu wa njia za kusafirishia umeme.

Alisema mradi huo unatakwia ukamilike kabla ya Machi 15 mwaka huu, na kusema mrdi huo ukienda kinyume na hapo serikali inaweza ikapata hasara na wafadhili wanaweza wakahitaji fedha zao.

Mgogoro huo ambao ulidumu kwa takribani zaidi ya miezi miwili baina ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Zakaria Kakobe kubisha kupitisha mradi huo kanisani hapo wka madai unamuathiri.

Na aliamua kutengeneza fulana maalum zinazovaliwa na waumini wa kanisa lake huku wakipiga kambi kanisani hapo kwa saa 24 kwa ajili ya kulinda kukabiliana na wafanyakazi wa TANESCO watakaokwenda kupitisha nguzo hapo.

Katika lindo hilo wafanyakazi wawili wa Tanesco waliweza kujeruhiwa walipofika kanisani hapo kuweka nguzo kupitihsa umeme huo.




 
Na Chondoma Shabani, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Fortunatus     Monday, March 08, 2010 12:33:19   
 
Serikali imefanya uamzi mzito ili kufanikisha maendeleo ya watanzania wengi wanao hitaji umeme.
 
 
Mtoa Maoni: MINA    Monday, March 08, 2010 12:38:15   
 
HAya sasa KAKOBE TUMA wafuasi wakampige WILLIAM NGEREJA ha ha hii ndio TANZANIA kweni momSO16 MNAMUONA MJINGA ANavyoomba msaada kwa UBUGUVU akanunue mizimu... haya sisi yetu amcho tu
 
 
Mtoa Maoni: moud     Monday, March 08, 2010 12:46:40   
 
Hapo serekali imefanya vizuri ili kumali malumbano na Kakobe. sasa naomba ni waulize wadau je Zakaria kakobe ni mtanzania halisi? na kama ni mtanzania kwa nini hataki kuelewa mpango waserekali ? na nifaida kwa jamii ya watanzania?
 
 
Mtoa Maoni: Dilly    Monday, March 08, 2010 12:53:45   
 
safi sana mahakama kwa mssuzi mazuri
 
 
Mtoa Maoni: dilly    Monday, March 08, 2010 12:55:48   
 
maamuzi mazuri
 
 
       Jumla kuna maoni (11), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Polisi kwa kete 300 za bangi
> Tani za mtama usiofaa wakamatwa Zanzibar
> Jeshi la Polisi laimarisha ulinzi Kariakoo
> Tendwa atupilia mbali pingamizi la Chadema
> Aangua kilio baada ya kutapeliwa- Kar iakoo
> Sheria isipofata mkondo wake, nitaandaa maandamano-Baswalehe
> Darasa la 7 waanza mitihani leo
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Chadema yawasilisha pingamizi
> Wanafunzi waweweseka Tabata
> Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma yateketea
> Ramli ya Joseph ilisema hivi!
> 7 papohapo, wengine majeruhi ajalini- Mabibo
> Makahaba msipotoshe vazi hili!
> Sakata la kugombania maiti bado tata
> Mahakamani kwa kujipatia ngono kwa njia ya madawa ya kulevya
> Chadema yamuwekea pingamizi Kikwete

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
9 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake