|
|
|
Mwanafunzi Mahakamani kwa wizi wa Mil.5 |

|
Monday, March 08, 2010 10:11 AM
Mwanafunzi Abdallah Miti [18] wa Shule ya Sekondari ya Ari iliyopo Tabata, amefikishwa katika Mahakama ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, kujibu tuhuma za wizi wa kuaminika wa Shilingi milioni 5
|
Mwanafunzi huyo alisomewa mashtaka mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Joyce Minde wa Mahakama hiyo.
Katuga alidai, mtuhumiwa alitenda kosa hilo, Februari 20, mwaka huu katika mtaa wa Garden Ilala jijini Dar es Salaam.
Katuga alidai mwanafunzi huyo aliiba fedha hizo kutoka katika gari namba T 630 aina ya Toyota mali ya Anselem Sigela. Mtuhumiwa alikana kuhusika na wizi huo na alirudishw rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa.
Ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika wendye uwezo wa kusaini shilingi milioni 5 mahakamani hapo.
Hivyo kesi hiyo iliahirishwa, itatajwa tena Machi 16, mwaka huu.
|
|
|
Na Pilly Kigome, Dar es Salaam
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
MINA
Monday, March 08, 2010 12:43:59
|
|
Mtoa Maoni:
Mchokozi
Monday, March 08, 2010 16:43:14
|
|
Mtoa Maoni:
KATUBA GF
Monday, March 08, 2010 21:44:20
|
|
Mtoa Maoni:
KATUBA GF
Monday, March 08, 2010 21:46:09
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Tuesday, March 09, 2010 00:21:49
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za Tanzania |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|