Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mwanafunzi Aiuza Bikira Yake Kwa Dola 32,000


Natalie Dylan, mwanamke aliyesababisha wimbi la wasichana kuzinadi bikira zao.
Thursday, February 04, 2010 4:01 AM
Mwanafunzi mmoja wa nchini New Zealand ameinadi bikira yake kwa dola 31,900 kwa mwanaume asiyemfahamu ili aweze kupata pesa za kulipia gharama za masomo yake ya chuo kikuu.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 aliinadi bikira yake kwenye mtandao wa www.ineed.co.nz baada ya kukabiliwa na ukata wa pesa.

Mwanafunzi huyo anayejiita "Unigirl" alijitambulisha kuwa yeye ni mrembo mwenye kuvutia, yuko fiti na mwenye afya njema.

Zaidi ya watu 1,000 walijaribu kuinunua bikira yake lakini mwanaume mmoja ambaye hakutajwa jina lake aliibuka mshindi baada ya kuweka dau kubwa la dola 31,900. (Takribani Tsh. Milioni 42).

"Nawashukuru watu wote zaidi ya 30,000 waliolitembelea tangazo langu, na zaidi ya watu 1,200 walioweka madau yao kuinunua bikira yangu", alisema mwanafunzi huyo.

"Dau lililoshinda ni kubwa sana kuliko hata nilivyotarajia".

Mwanafunzi huyo alisema kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na pesa atakazopata atazitumia kulipia masomo yake.

Mwanafunzi huyo aliendelea kusema kuwa ili mradi masuala ya afya yake yatapewa kipaumbele hana hiana kumtunuku bikira yake mwanaume yoyote yule bila kubagua kabila wala umri ilimradi apate pesa za kulipia masomo yake.

Mmiliki wa tovuti iliyotumika kuinadi bikira hiyo, Ross MacKenzie, alisema kuwa tangazo la mwanafunzi huyo lilikuwa ni halali kisheria na hakuna sheria yoyote iliyovunjwa.

Mwanafunzi huyo aligoma kufanya mahojiano na waandishi wa habari lakini MacKenzie, aliliambia gazeti la Waikato Times kuwa ameruhusiwa kutaja kiasi cha dau lililoshinda bila kutoa maelezo ya ziada.

Matukio ya wanawake kuzinadi bikira zao kwenye internet yaliibuka kwa kasi baada ya mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan ,22, kuinadi bikira yake na kupata mteja aliyeweka dau la dola milioni 3.7.

Natalie naye wakati anainadi bikira yake alitoa sababu kama hizi kuwa anatafuta pesa za kulipia masomo yake.

Mwezi mei mwaka jana nchini Ujerumani, mwanamke mmoja toka Romania, Alina Percea, 18, aliinadi bikira yake kwa matumaini ya kuingiza mamilioni kama Natalie lakini aliambulia euro 10,000 tu toka kwa mfanyabiashara wa Italia mwenye umri wa miaka 45 aliyeshinda katika mnada huo.

Mbali ya kupata dau dogo, Alina alipata hasara zaidi baada ya maafisa kodi wa Ujerumani kuzikata kodi pesa alizopata kwa kuinadi bikira yake akiambiwa kuwa alichofanya ni sawa na wanachofanya makahaba ambao nao wanalipa kodi kwa shughuli zao.

Alina alibakia na karibia nusu ya pesa alizopata baada ya makato ya kodi kufanyika.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: siso    Thursday, February 04, 2010 07:28:31   
 
hili tangazo sikuliona mapema lakini ninayo hakiba ya elfu kumi za tz nami ningeshiriki huu mnada
 
 
Mtoa Maoni: Ubuguvu    Thursday, February 04, 2010 09:46:19   
 
Umuhimu wa elimu mtu anauza mpaka vivyouzwa hapa tunajifunza kumbe hata majuu masomo wanalipia hakuna masomo ya buru na vile vile mwanafunzi unatakiwa ufaoye kazi kama hali yako ngumu ili uweze kujisomdsha Bikira zimekua dili sasa sijui imezidi nini au inaladha gani hili ntamuachia MKALIWAM atwambie maana sisi tumeoa wajane tumekuta zishachojolewa sijui hata ilivyo kaa lakini kutokana na haya matangazo kila siku na watu wanagombea hata mimi nafikiria kutafuta bikira lakini akubali kuolewa
 
 
Mtoa Maoni: DeClarkes    Thursday, February 04, 2010 09:46:30   
 
Nadhani hii ni style mpya ya kutafuta mapesa. Pole sana dada kwa matatizo na hatua uliyotumia kupata mafedha. Ila nadhani sio njia mbadala; Nadhani ikiwa ni hapa bongo basi ni just less than 1% watakuwa mabikra.
 
 
Mtoa Maoni: kitdu the great    Thursday, February 04, 2010 10:03:49   
 
Kwetu sheria zinasemaje? wanafunzi wetu wanaokosa mikopo wanaweza tumia njia hii kupata hela za kujisomesha?
Huenda serkali inakosa mapato kwa kutoliangalia suala hili na majangu doa wangeweza kuongeza pato la taifa kwani mapato yao ni makubwa kuliko watu wengi wanaofanya kazi za kawaida,

 
 
Mtoa Maoni: Cool sule    Thursday, February 04, 2010 12:24:45   
 
Huu upuuzi mtupu,binaadamu hata akifikia kuunadi utu wake kwenye internet amakuwa zaidi ya kuku mana kuku yy ananadiwa hajinadi.upuuzi mtupu na anwadhalilisha wanawake wenziwe
 
 
       Jumla kuna maoni (29), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..
> Baada ya Ajali Mtoto wa Miaka 3 Awa Chapombe na Mvutaji Sigara

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi