Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Paka Anayedaiwa Kuwa na Uwezo wa Kunusa Kifo Kabla Hakijatokea


Paka anayejulikana kwa jina la Oscar ambaye anadaiwa kunusa vifo vya wagonjwa mahututi
Wednesday, February 03, 2010 4:05 AM
Ukimuona ni paka wa kawaida ambaye hana tofauti yoyote na paka wengine lakini inasemwa kuwa ana uwezo wa kuwatambua wagonjwa wanaokaribia kufariki hospitalini na hadi sasa imesemwa kuwa ameishafanikiwa kuvinusa vifo vya wagonjwa 50 kabla hata havijatokea
Paka anayejulikana kwa jina la Oscar hujisogeza na kukaa karibu na kitanda cha mgonjwa aliyebakiza muda mchache kufariki.

Iwapo ndugu wa mgonjwa huyo watamfukuza paka huyo nje ya chumba cha mgonjwa wao na kumfungia mlango, basi paka huyo hugoma kuondoka na huanza kuukwaruza mlango kwa nguvu aking'ang'ania kuingia ndani.

Paka Oscar ambaye huishi katika nyumba moja ya kutunza wagonjwa wazee iliyopo kwenye mji wa Province katika jimbo la Rhode Island nchini Marekani hupenda kuzungukazunguka toka chumba kimoja hadi kingine katika nyumba hiyo.

Inadaiwa kuwa Paka Oscar huwa hapendi kutumia muda wake pamoja na vikongwe katika nyumba hiyo isipokuwa wale tu ambao wanakaribia kufariki.

Tabia ya paka huyo ambaye hivi sasa ana umri wa miaka mitano, iligunduliwa mwaka 2007 na manesi wa nyumba hiyo ambao kwa jinsi walivyo na uhakika na uwezo wa paka Oscar huwataarifu familia ya mgonjwa anayezungukiwa sana na paka huyo kuwa mambo yanaelekea kuwa mabaya.

Katika kuonyesha uwezo wa paka huyo, siku moja manesi walimchukua paka huyo na kumweka kwenye kitanda cha mgonjwa ambaye waliamini atafariki dakika yoyote ile, lakini paka huyo alichoropoka na kukimbilia chumba cha pili yake.

Uamuzi wa paka Oscar ulijionyesha siku hiyo hiyo kwa mgonjwa wa chumba cha pili kufariki siku hiyo hiyo jioni wakati mgonjwa wa chumba cha kwanza aliendelea kuishi kwa angalau siku mbili kabla ya kufariki paka Oscar akiwa amerudi pembeni ya kitanda chake.

Wataalamu hivi sasa wanamfanyia uchunguzi paka huyo ambaye alianza kulelewa kwenye hospitali hiyo tangia alipokuwa kichanga.

Mmmoja wa wanasayansi anayemfanyia uchunguzi paka huyo, Dr David Dosa, ameelezea mshangao wake kwa uwezo wa paka huyo kutabiri bila kukosea vifo vya wagonjwa 50 katika kipindi cha miaka mitano.

Dokta Dosa anasema kuwa hakuna maelezo yoyote ya kisayansi kuelezea tabia ya paka huyo.

Katika tukio jingine, mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Richards aliamua kukaa pembeni ya kitanda cha mama yake muda wote baada ya madaktari kumwambia kuwa mama yake aliyekuwa mgonjwa mahututi angefariki muda wowote ule.

Richard bila kupumzika alikaa pembeni ya kitanda cha mama yake kwa siku tatu mfululizo lakini mama yake hakufariki.

Madaktari walimshauri Richard aende nyumbani kwake akapumzike kidogo kabla ya kurudi baadae. Richard kwa shingo upande alikubali kuondoka kwenda kwake kupumzika.

Muda mfupi baada ya kuondoka, mama yake alifariki. Hakufariki akiwa peke yake bali Oscar alikuwa pembeni yake.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: hamisi    Wednesday, February 03, 2010 04:24:20   
 
aisee wazungu sayasi inawadanganya huyo paka ni jini waende tanga na mombasa waone paka walivyo zaidi ya huyo tena wanaongea
 
 
Mtoa Maoni: asmaa    Wednesday, February 03, 2010 08:12:34   
 
Uchawi upo na umetajwa kwenye vitabu vyote vya dini...ILA TUMESISITIZIWA TUSIUAMINI LAKIN UPO, NA MAJINI PIA YAPO..Ila tusiyape nguvu kushinda mwenyezimungu....Wazungu hawaamini mambo ya uchawi ila tuanweza sema huyo si paka bali ni JINI na hicho ndo chakula chake wangefanya uchunguzi je wakimuondoa kabsa kwenye hilo jengo idadi ya vifo vinakuaje???? Japo siku zao zimefika na hilo pia lakuangaliwa...

Na pia kiiman ni kwamba wanyama na watoto wachanga wanajua na kusikia mengi.

 
 
Mtoa Maoni: mkaliwam    Wednesday, February 03, 2010 09:19:20   
 
Aiaee hii kali,hivi angekuwepo hapa bongo ingekuwaje?naamini wageshampa sumu siku nyingi tu,kaka UBUGUVU nasikia na wewe una paka wako bwana anafanana na huyo sana tu
 
 
Mtoa Maoni: DeClarkes    Wednesday, February 03, 2010 09:33:08   
 
Jamani Mnashangaa nini mbona paka wa huku Bongo pia wakilia sana karibu na nyumba mnasema ni wanga! Nadhani labda inahitajika kusoma tabia za wanyama hawa maana anachofanya paka OSCAR sio tofauti na mipaka ya tunduru!
 
 
Mtoa Maoni: Matata    Wednesday, February 03, 2010 09:42:39   
 
Ni pale tu tutakapokubali kuwa viumbe vingine kama paka huyu vinauwezo ambao bado hatuufahamy ndipo Maneno kama Uchawi, Jini na Misukule vitaondoka. Tafuta katika mtandao au angalia picha za Haiti ni mbwa wangapi walikufa? Hao mbwa walijuaje tetemeko litatokea?
 
 
       Jumla kuna maoni (19), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..
> Baada ya Ajali Mtoto wa Miaka 3 Awa Chapombe na Mvutaji Sigara

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi