Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Ana Miaka 13 Lakini Anaonekana Kama Bibi wa Miaka 50


Mtoto Zara mwenye umri wa miaka 13
Wednesday, February 03, 2010 2:44 AM
Akikuambia kuwa ana umri wa miaka 13 unaweza ukabisha mpaka siku inayofuatia bila kukubali, msichana Zara Hartshorn wa nchini Uingereza aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu anashindwa kuufaidi utoto wake kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia kuwa yeye ni bibi mwenye umri wa miaka zaidi ya 50
Siku moja Zara Hartshorn alipanda basi la abiria na kutaka kukata tiketi ya watoto lakini dereva wa basi hilo alimuangalia kwa mshangao na kumwambia kuwa asifanye masihara alipe pesa kamili.

Zara aliposema kuwa yeye ni mtoto na ana umri wa miaka 13, dereva huyo ambaye alikuwa ni mzee wa makamo, alicheka sana na kumwambia kama ndio hivyo basi na mimi nina umri wa miaka 21.

Abiria nao waliingia kwenye mjadala huo na kumuunga mkono dereva kuwa Zara anawachezea watu akili kwani anaonekana wazi kuwa yeye ni kikongwe mwenye wajukuu.

Zara kwa aibu alishuka toka kwenye basi hilo na kusubiria basi jingine kwa imani dereva wa basi lifuatalo angeweza kumuelewa kuwa yeye ni mtoto.

Huo ni mkasa mdogo sana kati ya mikasa inayomkumba binti Zara Hartshorn wa Rotherham nchini Uingereza ambaye umri wake halisi ni miaka 13 pamoja na kwamba anaonekana kuwa na umri zaidi ya miaka 50.

Zara anakabiliwa na ugonjwa unaoitwa lipodystrophy ambao humfanya aonekane mzee sana kuliko umri wake huku akiwa na tabia za kitoto kama watoto wenzake.

Mama yake Zara bi Tracey Pollard ilibidi achukue uamuzi wa kumsimamisha masomo Zara kwakuwa alikuwa akitaniwa sana na wenzake akiitwa "Bibi" na kubandikwa majina kadhaa ya fedheha.

Ugonjwa unaomkabili Zara umewahi kuwatokea watu 2,000 tu duniani ambapo tabaka la chini la mafuta la ngozi hutoweka na kuifanya ngozi izeeke kwa spidi ya ajabu sana.

Ugonjwa wa lipodystrophy hauna tiba hivyo Zara ataendelea kuzeeka mapema jinsi anavyozidi kuendelea kukua.

Zara amerithi ugonjwa huo toka kwa mama yake ambaye ni miongoni mwa wagonjwa wachache sana duniani wa ugonjwa huo.

"Nilijuta kumzaa Zara, nilihuzunishwa sana nikifikiria kuwa Zara atapitia matatizo yote yaliyonikumba mimi wakati wa utoto wangu", alisema mama yake Zara.

Zara anaelezea masikitiko yake kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia na kumtania kwa kusema kuwa wakati mwingine hukimbilia chumbani kwake na kuanza kulia peke yake.

Chini ni VIDEO na linki ya picha za Zara.
  GONGA HAPA KWA PICHA ZA MTOTO ZARA NA UTU UZIMA WAKE  


VIDEO - Ana Miaka 13 Lakini Anaonekana Kama Bibi wa Miaka 50





 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: moms016    Wednesday, February 03, 2010 02:52:14   
 
OMG pole sana! inasikitisha, neno pekee la kusema "kujafa hujaumbika"
 
 
Mtoa Maoni: Semenya    Wednesday, February 03, 2010 03:04:40   
 
Duh!!!!!!!! kwa kweli inasikitisha sana ss akifika hy miaka 50 atakuaje.

pole sana zara u must be feeling so down lakini mambo ya maradthi tena hayo tunakuombea Mungu akurahisishie misukosuko Amina.

 
 
Mtoa Maoni: Cinderella    Wednesday, February 03, 2010 03:20:11   
 
pole sana ni kweli hujafa hujaumbika
 
 
Mtoa Maoni: mkaliwam    Wednesday, February 03, 2010 09:22:07   
 
Pole sana yote ni mipango ya mungu
 
 
Mtoa Maoni: zhao    Wednesday, February 03, 2010 10:05:25   
 
kumbe na wao piahuchekana?duuu pole dada
 
 
       Jumla kuna maoni (14), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake