Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Kibonge wa Dunia Apungua Kilo 127,Lakini Bado Anaongoza


Paul Mason alivyokuwa awali
Tuesday, February 02, 2010 2:06 AM
Mtu mnene kuliko wote duniani amepungua kilo 127 baada ya kufanyiwa operesheni ya kuokoa maisha yake lakini bado ameendelea kutambulika kama mtu mnene kuliko wote duniani kwa kilo zake 311 zilizobaki.
Baada ya kupungua kilo 127, Mtu mnene kuliko wote duniani, Muingereza Paul Mason hivi sasa ana uzito wa kilo 311 na ameendelea kushikilia taji la unene duniani.

Mason mwenye umri wa miaka 48, alitumia mwisho wa wiki kwenye kitanda cha kitengo maalumu cha hospitali baada ya kufanyiwa operesheni kubwa ya kumzuia kuendelea kunenepa na kuondolewa kwa mafuta kwenye tumbo lake.

Katika operesheni hiyo tumbo la Mason lilipasuliwa na kutengenezwa kisehemu kidogo kama pochi kwaajili ya kuhifadhi chakula chake.

Kwa maana hiyo chakula chake chote hivi sasa kitaenda kwenye hicho kipochi na hivyo kumfanya awe anakula kiasi kidogo sana cha chakula.

Wiki iliyopita madaktari walimuingiza Mason kwenye diet ya nguvu ya kuupunguza unene wake ili aweze kuwa fiti kwaajili ya operesheni.

Mason ameelezea nia yake ya kupunguza uzito wake zaidi ili aweze kuendesha gari.

Mwaka 2002 kutokana na unene wa Mason, Zimamoto iliwabidi waubomoe ukuta wa chumba chake na kisha kutumia forklift ili kuweza kumbeba na kumwingiza kwenye ambulansi kumwahisha hospitali kwaajili ya operesheni ya hernia.

Wakati huo alikuwa na uzito wa kilo 355, aliwaambia madaktari kuwa anataka kupunguza uzito wake lakini alianza kula sana ili kuvunja rekodi ya dunia awe mtu mnene kuliko wote duniani.

Hatimaye mwaka jana alifanikiwa kuvunja rekodi hiyo kwa kufikisha uzito wa kilo 444 na kumfunika kibonge wa dunia wa wakati huo toka Mexico, Manuel Uribe ambaye aliamua kupunguza uzito wake ili aweze kumuoa mpenzi wake.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Cinderella    Tuesday, February 02, 2010 02:53:59   
 
unene nao hauna maana jamani!!!!!!!!!!!!
 
 
Mtoa Maoni: TAMARIN    Tuesday, February 02, 2010 09:44:59   
 
Safi sana kibonge endelea na msosi wa nguvu ili uweke rekodi kama misri
 
 
Mtoa Maoni: NGUZO    Tuesday, February 02, 2010 19:18:12   
 
Duuh!!!!!!! kuna watu wanene duniani
 
 
Mtoa Maoni: KING    Tuesday, February 02, 2010 20:04:24   
 
C bure ni mgonjwa huyu, uzito wote huo aliupata vp? Kweli ulimwengu una vijimambo, lkn nampa hongera Bw. Mason kwa kufanikiwa ktk operation aliyofanyiwa. Cha msingi afuate maagizo ya madaktari kuboresha afya yake na kupungua uzito zaidi ili siku ndoto yake ya kuendesha gari itimie.
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Wednesday, February 03, 2010 01:20:34   
 
Mungu anaumba atakavyo! Penye nia pana uwezekano, iwapo kweli amekusudia kujipunguza tunamtakia mafanikio.. Ila tu kwa wadau wote mazoezi muhimu alau mara moja kwa wiki!


 
 
       Jumla kuna maoni (8), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake