Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Kufanya Operesheni Ili Afanane na Supastaa wa Marekani


Nyota wa Marekani, Jessica Alba
Monday, February 01, 2010 4:56 AM
Ili kumfanya mpenzi wake wa zamani amrudie tena, mwanamke mmoja wa nchini China anafanya operesheni ya kuubadilisha mwili wake ili afanane na nyota wa Marekani, Jessica Alba.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 21 aliyejitambulisha kwa jina la Xiaoqing wa nchini China ameamua kufanya operesheni ya kuubadilisha mwili wake ili afananane na mcheza sinema wa Marekani, Jessica Alba.

Mwanamke huyo aliliambia gazeti la Shanghai Daily kuwa ameishakutana na madaktari wa operesheni za urembo wa mjini Shanghai ambao wamemuahidi watamfanyia operesheni hiyo bure.

Xiaoqing aliliambia gazeti hilo kuwa atafanya operesheni za kuubadilisha mwili wake ili afanane na Jessica Alba kwakuwa mpenzi wake wa zamani anampenda sana mcheza sinema huyo hivyo anaamini kuwa atakapofanana naye basi mpenzi wake atamrudia.

Afisa wa hospitali ya Shanghai Time Plastic Surgery Hospital, ambayo Xiaoqing atafanyiwa operesheni zake alisema kuwa Xiaoqing atafanyiwa bure operesheni za kurekebisha kope na nyusi za macho yake pamoja na operesheni ya pua yake ili aweze kufanana na Jessica Alba ambaye alitamba kwenye "Sin City" na "Fantastic Four".

"Hakuna wasiwasi wa malipo, operesheni inawezekana kufanyika", alisema afisa huyo na kuongeza "Inabidi afahamu kuwa hataweza kuirudia sura yake ya zamani baada ya operesheni".

Xiaoqing alisema kuwa mpenzi wake huyo wa zamani anampenda sana Jessica Alba kiasi cha kwamba kwenye ukuta wa chumba chake ameweka picha yake kubwa na hata kwenye simu yake kuna picha za msanii huyo maarufu wa Marekani.

Xiaoqing aliongeza kuwa mpenzi wake huyo alikuwa akimlazimisha ajipodoe kama Alba na alimnunulia wigi ambalo alimtaka alivae wakati wote. Xiaoqing alisema kuwa uhusiano wao ulivunjika baada ya kuamua kulivua wigi hilo na kulitupa.

"Nampenda sana ndio maana nafanya hivi... sitaki kumpoteza ", alimalizia kusema Xiaoqing.

 
Source: AFP    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Trymore    Monday, February 01, 2010 07:37:04   
 
Jamani, huu ndo ulimbukeni wa mapenzi, yaani ujibadili ili tu kurudiwa? Are u not proud of yourself who and what u are?
Na asiporejesha penzi?
Huyo jamaa wala hakupendi, kama angekupenda isingekuwa lazima akuache, eti kisa umekataa kuvaa wigi kama la Jessica Alba
...ngoja nicheke kidogo hahahhhhaaaaaaaaah...
pole dada wa kichina!

 
 
Mtoa Maoni: Ubuguvu    Monday, February 01, 2010 08:05:43   
 
Mimi ninawasi wasi na huu upasuaji kwanini hawa madaktali wakubali bure au wanataka kujifunzia huwezi kufanyiwa plastic surgery (amaliatu tajimili) bure alafu akipata madhala atashitaki hospitali nadhani alipaswa kifikiria madhala atakae yapata hapo badae kabla hajafanya plasic surgery kufanya upasuaji wa urembe chini ya miaka 35 madhala yake nimakubwa zaidi kwa sababu mwili unakua bado upo katika mabadiliko ukifanya bure leo kwa hiyari bada ya mwaka 1 utafanya na pesa lazima hakuna hata mt
 
 
Mtoa Maoni: spy    Monday, February 01, 2010 09:26:42   
 
kumbe ubuguvu anaishi arabuni!!!!!!
 
 
Mtoa Maoni: pili    Monday, February 01, 2010 10:05:32   
 
huyu dada hajui anachokitaka. kwa taarifa yake hapendwi na huyo kijeba wake. angempenda basi asingemfanya awe kama mtu mwingine.
hivi ndo kwanza kabinti,akifanyiwa hio po nahis after 2 yrs atakua kituko.

 
 
Mtoa Maoni: moms016    Monday, February 01, 2010 13:54:09   
 
Mm naungana na wote walionitangulia kimaoni na mawazo yao sawa, Nijuavyo ktk mapenzi ni kuwa "mpende mpenzi wako km alivyo (ktk uhalisi wa maumbile yake)" ama kupenda kwa kushartisha uwe hivi uwe vile ni ishara ndg ya mapenzi, na hii km mapenzi yenyewe yapo.
Mm naona huyu dada Xiaoqing, apige moyo konde aachane na huyo kjn wake na asubirie mengine (ingawa w`me wachache na bidhaa adimu sana(KIPARA)).

MINA hata uwe km REMMY nakupenda tu.. meno km reki! nakupenda tu..
kipofu.. twende!


 
 
       Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake