Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mwanaume Mwingine Apata Mimba, Kujifungua Mwezi Ujao


Scott Moore kushoto akiwa na mumewe Thomas kulia
Wednesday, January 27, 2010 2:14 AM
Mwanaume wa nchini Marekani ambaye alizaliwa kama mwanamke kabla ya kubadili jinsia yake kuwa mwanaume anatarajia kujifungua mtoto wa kiume mwezi ujao.
Scott Moore mwanaume wa nchini Marekani ambaye alizaliwa kama mwanamke anatarajia kuwa mwanaume wa pili wa nchini Marekani kupata mimba na kujifungua mtoto.

Scott anatarajia kujifungua mtoto wa kiume mwezi ujao.

Mume wa Scott ambaye naye alizaliwa mwanamke kabla ya kubadilisha jinsia na kubadilisha nyeti zake, anatarajia kuwa pembeni ya Scott wakati wa kujifungua.

Scott amejibadilisha jinsia kuwa mwanaume lakini alikubaliwa kuolewa kisheria na Thomas kwa kutumia cheti chake cha kuzaliwa ambacho kinamuonyesha kuwa yeye ni mwanamke.

Thomas yeye anahesabika mwanaume kwakuwa alibadilisha jinsia yake na kufanya operesheni ya kuuondoa uke na kuupandikiza uume.

Scott yeye bado hajafanya operesheni hiyo ya kuuondoa uke wake hivyo bado ana sehemu za siri za kike.

"Tunajua watu watatukosoa lakini sisi tuna furaha ya kupata mtoto na wala hatujisikii vibaya", alisema Scott mwenye umri wa miaka 30 ambaye alisema mtoto wao wamepanga kumpa jina la Miles.

Scott anasema kwamba alizaliwa kama mwanamke akipewa jina la Jessica na alianza kupata shauku ya kuwa mwanaume alipoanza kupevuka alipokuwa na umri wa miaka 11.

Scott aliendelea kusema kuwa wazazi wake awali walimpinga lakini baadae walimsaidia kutimiza nia yake ya kuwa mwanaume.

Alianza kumeza vidonge vya homoni za kiume alipokuwa na umri wa miaka 16 na wazazi wake walimlipia gharama za kuyaondoa matiti yake.

Scott anasema kuwa alishindwa kulipia gharama za operesheni ya kuutoa uke wake na kuupandikiza uume hivyo hadi leo bado ana sehemu za siri za kike.

Thomas kwa upande wake yeye alifanikiwa kufanya operesheni ya kuuondoa uke na kuupandikiza uume mwaka jana.

Scott alipata ujauzito baada ya kupandikizwa mbegu za kiume za mwanaume ambaye yuko karibu na familia hiyo.

Scott anasema kuwa ana mpango wa kumzaa mtoto wake kwa njia ya asili.

"Hatukutaka kuwashtua watu watakapoona mwanaume anajitokeza kuja kujifungua", alisema Scott akielezea jinsi walivyomtafuta daktari wa kumzalisha.

Scott anasema kuwa hawakumpata kirahisi daktari huyo kwani madaktari wengi walikuwa wakikwepa kuonana naye na hata kumpa matibabu.

"Tunataka kuwaonyesha watu kuwa watu waliobadilisha jinsia nao wanaweza kuanzisha familia zilizojaa upendo na furaha", alisema Thomas.

 
Source: Mail Online    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: mdau    Wednesday, January 27, 2010 03:15:28   
 
The world is caming to an end,enzi za marehem bibi hayakuwepo haya.
 
 
Mtoa Maoni: Cinderella    Wednesday, January 27, 2010 03:21:10   
 
LOL mdau usinichekeshe enzi za marehemu bibi sio?
 
 
Mtoa Maoni: Mchafukoge    Wednesday, January 27, 2010 03:49:59   
 
Haya wanaoshindana na M/mungu baki na wanaoshinda na dunia baki, tulikotoka mbali tuendako karibu.....kazi kweli2
 
 
Mtoa Maoni: Trymore    Wednesday, January 27, 2010 06:20:05   
 
mmmh!
Binadamu tunaelekea wapi jamani?
Mbona tunashindana na Mungu wakati tuna matatizo mengi ya msingi ya kuyafanyia kazi?

 
 
Mtoa Maoni: Mwanza boy    Wednesday, January 27, 2010 06:45:33   
 
Namhurumia mwana atakayezaliwa!!
 
 
       Jumla kuna maoni (33), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake