Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mume Mkware Ala Uroda na Mama Mkwe Wake


Irene Whitelaw
Monday, January 25, 2010 7:39 AM
Mume mkware wa nchini Uingereza ambaye alisamehewa na mkewe baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mama mkwe wake, amemkimbia mkewe na kwenda kuishi na rafiki wa mke wake.
Marafiki wa mwanamama wa Kiingereza, Irene Whitelaw,35, hawakuamini masikio yao waliposikia Irene amemsamehe mumewe ambaye alikuwa akifanya mapenzi na mama yake mzazi.

Mume wa Irene, Andy Simpson mwenye umri wa miaka 42 alianza uhusiano wa kimapenzi na mama mkwe wake ambaye alihamia kwenye nyumba yao baada ya mumewe kufariki mwaka 2000.

Mama yake Irene, Marlene mwenye umri wa miaka 60 alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Andy kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ya Irene kugundua.

Irene alisema kuwa kabla ya kuoana na Andy, mama yake alikuwa hapatani kabisa na Andy na alikuwa hataki aolewe naye.

Lakini baada ya baba yake kufariki mwaka 2000, mama yake alihamia nyumbani kwake na kuanza kumsaidia kulea watoto wake wawili. Haukupita muda mrefu Andy alikuwa karibu zaidi na mama mkwe wake ambaye awali walikuwa hawapatani kama panya na paka.

Siku moja Irene alirudi nyumbani na kukuta ujumbe ambao mama yake alimuandikia Andy akimuelezea mipango ya kutoroka naye na kwenda kuishi naye pamoja. Upande wa pili Andy alimwambia mama mkwe wake kuwa afanye mambo kwa uangalifu ili Irene asishtukie.

Irene alipombana mama yake kuhusiana na ujumbe huo, alishangazwa na majibu aliyopewa na mama yake ambaye alisema "Mimi nipo fiti zaidi yako kitandani ndio maana Andy ananipenda zaidi".

Irene kwa hasira alichukua watoto wake na kuhamia kwa ndugu zake ambao nao walimwambia kuwa walikuwa wakijua uhusiano wa mama yake na Andy lakini walikuwa hawajui watamueleza vipi.

Baada ya kusikia taarifa ya Andy kuwa alijaribu kujiua baada ya siri hiyo kufichuka, Irene aliamua kumsamehe.

Irene alipiga moyo konde kwa kuwafikiria watoto wake na kuamua kuanza maisha mapya na Andy katika mji wa Glasgow, Scotland.

Haukuchukua muda mrefu Andy aliisaliti tena ndoa yake na kuanza uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa mkewe jirani yao Lynn McNab, 42.

Siku ambayo Irene aligundua uhusiano wao, Andy aliamua kuondoka na kuhamia kabisa kwenye nyumba ya Lynn ambaye alikuwa akiishi peke yake na watoto wake watano.

Kwa fedheha aliyokuwa akipata kumuona mumewe akijitawala na rafiki yake nyumba ya jirani, Irene aliamua kuhama mtaa na kuhamia eneo jingine.

Irene ambaye anasema amevunjika moyo na hana imani tena kwa wanaume, amekuwa akiwaelezea watoto wake "baba yenu alitembea na bibi yenu ndio maana tukaachana".

Irene anasema kuwa hivi sasa anajaribu kujifunza kuwaamini tena wanaume ili aweze kuutunza uhusiano wake mpya na mwanaume ambaye ametangaza ndoa.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: DeClarkes    Monday, January 25, 2010 09:13:55   
 
Huu ni unyama, ni la kushangaza kwa mtu kufanya ng'ono kama mmbwa! Ni ajabu na kweli, lakini na wanawake wachague sio wanakula kila kitu!
 
 
Mtoa Maoni: KING    Monday, January 25, 2010 10:34:30   
 
What an infidelity! Hakika Bi. Irene ni mke mwema na mvumilivu hasa ila ana balaa la mume na mama. Kosa kubwa ni la mama mkwe hapo, hv inaingia vp akilini mtu kutembea na mme wa mtoto wako? Alianzia wapi huyu? Huu ni ukatil mkubwa sana, hv Bi. Irene alijisikia vp baada ya kuligundua hili, mama mzazi? Hapana, huu ni ufirauni na tabia za fisi. Katu c ubinadamu. Nachelea kusema M/MUNGU alipelea kumuumba binadamu Bi. Marlene. Katu Andy c mtu wa kuwa mume wa binti yeyote. LAANA YA MOLA IWASHUKIE
 
 
Mtoa Maoni: mark.mushi    Monday, January 25, 2010 15:20:13   
 
msanii wa bongoflava na producer mtarajiwa bado niko sijafulia duh ata ningekuwa mimi ningekula vitu kama mama mkwe analipa na anataka ahah kwanini nisichomeke ndani?sijafulia niko ila nitarudi tu kwa fujocku1,ubuguvu ujo?watu wanakula mapacha,mtu na sister wake,adi maza mdogo,aunt sembuse yee big up nakuunga mkono,
 
 
Mtoa Maoni: chukulubu    Monday, January 25, 2010 18:22:07   
 
mark mushi haya maneno yako au wamekuonea,nafikiri hujatulia unahitaji upewe sebuleni party.maana maneno hayo hapo juu hayalingani na mtu mwenye hekima ambaye ni kiongozi wa kesho.
 
 
Mtoa Maoni: Dilly    Monday, January 25, 2010 19:02:49   
 
King usimtese Wende tafadhali hayo mambo siyo mazuri sana ya kwenda hadi kwa mama mkwe.
Dah!! Dunia imekwisha walah!!

Mina Bhai utaratibu huo hatuna kwanza kwa mila na desturi za akina Bhai akiamatwa mtu anafanya mapenzi na mama Mkwe anapigwa fimbo laki moja hadharan, halafu anatahiliwa tena

 
 
       Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..
> Baada ya Ajali Mtoto wa Miaka 3 Awa Chapombe na Mvutaji Sigara

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi