|
|
|
VIDEO - Msichana wa India Anayevuja Damu Mara 50 Kwa Siku |

Twinkle Dwivedi katika hali yake ambayo humtokea kila siku takribani mara 50 |
Thursday, January 21, 2010 2:17 AM
Msichana Twinkle Dwivedi mwenye umri wa miaka 14 wa nchini India anasumbuliwa na ugonjwa ambao umewafanya madaktari wakune vichwa sana bila majibu. Mwili wa Twinkle huvuja damu mara 50 kwa siku kupitia kwenye macho yake, pua, masikio na kwenye nyayo zake. |
Bila ya kuwa na kidonda chochote wala mchubuko wowote, msichana wa kihindi Twinkle Dwivedi, 14, huvuja damu mara 50 kwa siku.
Twinkle hutoa machozi ya damu, damu humiminika toka kwenye kichwa chake, shingoni, masikioni, puani na kwenye nyayo zake.
Kutokana na kupoteza damu nyingi sana zinazovuja bila sababu yoyote kupitia kwenye ngozi yake, Twinkle aliwahi kuwekewa dripu ya damu.
"Huwa sisikii maumivu yoyote wakati damu zinapoanza kuchuruzika lakini hunifanya niwe mchovu na wakati mwingine huwa na maumivu ya kichwa", alisema Twinkle.
Dr George Buchanan, daktari mtaalamu wa masuala ya damu toka Marekani alisafiri hadi India kwenda kujaribu kugundua ni kitu gani kinachomsibu Twinkle.
Dokta Buchanan alibaki hana jibu la kutoa baada ya kushuhudia damu zikivuja toka kichwani na kwenye viganja vya mikono ya Twinkle bila ya Twinkle kuwa na mchubuko wowote.
Wataalamu wanaomfanyia uchunguzi Twinkle kujua kinachomsibu wamepanga kuweka kamera za ulinzi zitakazomrekodi Twinkle kwa ukaribu zaidi ili kujua jinsi damu hizo zinavyoanza kutoka kwenye ngozi yake.
Mwaka jana kijana wa Kimarekani Calvino Inman, 16, toka Rockwood, Tennessee, naye alianza kutoa machozi ya damu na hadi sasa anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wake ambao haujajulikana ni ugonjwa gani.
Chini ni VIDEO inayomuonyesha Twinkle akivuja damu toka sehemu mbali mbali za mwili wake. |
|
|
VIDEO - Msichana wa India Anayevuja Damu Mara 50 Kwa Siku
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Thursday, January 21, 2010 02:37:06
|
|
Mtoa Maoni:
m2 mzima berny
Thursday, January 21, 2010 08:58:38
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Thursday, January 21, 2010 11:00:26
|
|
Mtoa Maoni:
Bhai.
Thursday, January 21, 2010 12:21:58
|
|
Mtoa Maoni:
Dilly
Thursday, January 21, 2010 15:39:48
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (8), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
More life style news and articles |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|