Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Makalio na Mapaja Makubwa ni Bora Kwa Afya


Wednesday, January 13, 2010 4:44 AM
Wanawake wenye makalio makubwa na mapaja makubwa kama vile Beyonce na Jeniffer Lopez wana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa ya moyo na kisukari kulinganisha na wanawake wenye makalio madogo, matokeo ya utafiti wa wanasayansi nchini Uingereza umeonyesha.
Wanasayansi wa nchini Uingereza waliofanya utafiti wao katika chuo kikuu cha Oxford University wamegundua kuwa makalio makubwa yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko matumbo makubwa (vitambi).

Utafiti umeonyesha kuwa makalio na mapaja makubwa huhifadhi mafuta ambayo husaidia mwili kujilinda na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.

"Mafuta ya kwenye makalio na mapaja ni bora kwa afya lakini mafuta mengi ya kwenye tumbo si mazuri kiafya", alisema Dr Konstantinos Manolopoulos, mmoja wa watafiti watatu walioshiriki kwenye utafiti huo ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la International Journal of Obesity.

Watafiti hao walisema kwamba mafuta ya kwenye tumbo hutoa tindikali nyingi za mafuta zenye madhara kwa mwili wakati mafuta ya kwenye makalio na mapaja huzuia tindikali za mafuta zenye madhara kuingia kwenye misuli na maini na hivyo kuuepusha mwili na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.

Ingawa mafuta ya kwenye makalio na mapaja huyeyuka taratibu sana lakini mafuta hayo hutoa homoni zenye faida zijulikanazo kama adiponectin ambazo huilinda mishipa ya damu na kusimamia kiwango cha sukari mwilini.

Wanasayansi hao walisema kuwa wanaendelea na utafiti ili kutengeneza dawa za kuufanya mwili uhifadhi mafuta yake kwenye makalio na mapaja ili kupunguza matatizo ya kiafya yanayosababishwa mafuta kujazana kwenye tumbo.

Utafiti huo ulimalizia kwa kusema kuwa wanawake wenye mapaja au makalio madogo sana wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo kadhaa ya kiafya kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Leo    Wednesday, January 13, 2010 05:25:04   
 
Nina jambo linanisumbua hapa kidogo..kwa mfano huku kwetu afrika wanawake huwa wana makalio makubwa kuliko wanaume, hivyo tunaweza kusema wanaume wako kwenye risk ya haya magonjwa zaidi?
 
 
Mtoa Maoni: tumbo    Wednesday, January 13, 2010 06:55:30   
 
wamekuambia ni wanawake....! sasa wanaume tena wa nini....? muwe waelewa.
 
 
Mtoa Maoni: WA-CHANIKA    Wednesday, January 13, 2010 07:32:39   
 
Hizi tafiti zinazidi kuwa nyingi sasa zina nipa wasiwasi ukweli wake. Na kwa wale wenye matako ya kutengeneza kwa dawa za kichina hapo vipi??
 
 
Mtoa Maoni: Ubuguvu    Wednesday, January 13, 2010 09:06:34   
 
Dada zangu wa bongo musiufahamu vibaya huu utafiti makalio makubwa wanayokusudiwa hapa ni yale ya asiri tu sio yale yakutumia dawa za china kamaji matu sehemu imevimba ukigusa kama inabonyea kama godoro la sufi makali haya hayamo na yanamadhala makubwa yanaufanya mwili usiweze kishika sawa sawa mwanamke hatakua na taiti hole
 
 
Mtoa Maoni: Mchafukoge    Wednesday, January 13, 2010 09:24:45   
 
Sasa hizi tafiti zinazidi kuwa nyingi au ndio tuseme kila wasomi wanakuja na tafiti zao, mwishowe wataleta faida za kuwa na nanihii kuubwa.....maana naona tuendako karibu kuliko tutokako?

Mnataka kufanya wadada waanze kutumia chemicals kwa wiingii.

 
 
       Jumla kuna maoni (29), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake