|
|
|
Banana Zoro Aahidi Kuonyesha Makali Yake Mwaka Huu |

MWANAMUZIKI na mmiliki wa bendi ya B-Band, Banana Zahir Ally Zorro |
Tuesday, January 12, 2010 10:17 PM
MWANAMUZIKI na mmiliki wa bendi ya B-Band, Banana Zahir Ally Zorro ametamba kuwa wanamuziki wa bendi yake akiwemo baba yake mzee Zorro wamejipanga vyema mwaka huu kuhakikisha wanatamba katika medani ya muziki nchini. |
Akizungumza na Nifahamishe.com, Banana alisema kuwa mwaka 2009 bendi yake imefanya kazi kubwa na imeweza kuzikonga vilivyo nyoyo za wapenzi wa muziki waliohudhuria katika maonyesho yao.
Banana alisema pamoja na kazi hiyo, lakini mwaka 2010 wanataka kuhakikisha kuwa wanafanya kazi ambayo itawavutia wadau wote wa muziki.
"Unajua sisi lengo letu ni kuwa juu kila wakati. Kwa kuwa mwaka 2009 tumeweza kufanya vyema, hatutaki kuridhika na mafanikio hayo. Tunataka kupiga hatua zaidi na kuwa bendi tishio nchini," alisema Banana.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa anaamini hilo litatimia kwani wanamuziki wake akiwemo baba yake Mzee Zahir Ally Zorro ni watu wa kujituma na wenye kiu ya mafanikio.
"Ndani ya B- Band hakuna bosi. Kila mmoja ana kiu ya kuona tunapiga hatua zaidi, ndiyo maana hata ukija kwenye maonyesho yetu unaona namna baba yangu anavyojituma na kuwa sawa na vijana wengine" alisema Banana.
Banana alisema baada ya kutamba na vibao kama Nzela katika mwaka wa 2009, mwaka huu wanatarajia kutoa vibao vingi vipya na kujigamba kuwa anaamini vibao hivyo vitafanya vyema. |
|
|
Na Kalimanzila, Dar
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Wednesday, January 13, 2010 00:12:53
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Wednesday, January 13, 2010 03:14:05
|
|
Mtoa Maoni:
KING
Wednesday, January 13, 2010 18:04:32
|
|
Mtoa Maoni:
Dilly
Friday, January 15, 2010 09:00:53
|
|
Mtoa Maoni:
MINA
Friday, January 15, 2010 10:14:12
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za burudani |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|