Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
'Rambo' Avunjika Shingo Wakati wa Kuigiza Filamu


Sylvester Stallone au maarufu kama "Rambo"
Thursday, January 07, 2010 12:34 AM
Nguli wa filamu za kibabe Sylvester Stallone au maarufu kama Rambo amevunjika shingo katika mojawapo ya mapambano yaliyopo katika filamu yake mpya ya 'The Expendables'.
Sylvester Stallone au maarufu kama "Rambo" amevunjika shingo katika mojawapo ya seti za filamu yake mpya "The Expandables" ambayo inatarajiwa kuingia kwenye kumbi za sinema katikati ya mwaka huu.

Katika filamu hiyo inayotarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali Rambo mwenye umri wa miaka 63 amewashirikisha wasanii wengi maarufu kama vile Arnold Schwarzenegger, 62, Bruce Willis, 54, Dolph Lundgren, 52, Mickey Rourke, 57, Jet Li, 46, na Jason Statham, 37.

Rambo alivunjika shingo wakati alipokuwa akipigana na mbabe wa mieleka Stone Cold Steve Austin na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa dharura na kuwekewa vyuma kwenye shingo yake.

Rambo alisema kuwa mpambano wake na Austin kwenye seti ya filamu hiyo ulikaribia kuwa sawa na mpambano wa kweli ambapo aliangushwa vibaya na kuvunjika shingo yake.

Hii si mara ya kwanza kwa Rambo kuumia wakati wa kuigiza filamu. Mwaka 1985 Rambo aliwahishwa hospitali kwa helikopta baada ya kupewa ngumi nzito ya mbavu na Dolph Lundgren ambaye aliwika sana wakati wa filamu ya "Red Scorpion".

Hivi karibuni Rambo alitangaza kuwa uhasimu wake na Arnold Schwarzenegger katika filamu za Action umeisha na sasa ni marafiki.

"Ingawa alikuwa hasimu wangu mkubwa wakati huo, hivi sasa ni rafiki yangu mkubwa wa karibu", alisema Rambo.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: moms016    Thursday, January 07, 2010 01:34:29   
 
Dah kumbe ss ni wa zamani, basi tu!
AJALI KAZINI, MTEMBEA NA JUA C MKAA NDANI! YOTE MAISHA, POLE SANA MSANII RAMBO, UNAKUBALIKA. HLF INAONEKANA FILAMU LAKE LITAFUNGA MTAA MANAKE MASTAA WENGI TU.
UBUGUVU unitafute kwa wkt wako nikupe mistari juu ya RAMBO nina uhakika asilimia 3000 (elfu tatu) humjui..

 
 
Mtoa Maoni: Noel    Thursday, January 07, 2010 03:49:28   
 
Jamaa wanapigana kikweli kweli mpaka wanaumia sio mastaa wetu wakina kanumba na maximo wao wanaruka ruka tu
 
 
Mtoa Maoni: MAHADHI ALLI    Thursday, January 07, 2010 08:55:34   
 
Mimi namkubali Rambo maana filamu zake zote zinnikosha. Sina budi kumpa pole za dhati kwa kuumia shingo
 
 
Mtoa Maoni: soud    Thursday, January 07, 2010 09:14:09   
 
pole sana Rambo sina zaidi la kusema
 
 
Mtoa Maoni: DeClarkes    Thursday, January 07, 2010 09:35:27   
 
Pole sana Rambo; lakini nadhani watu walioamua kuweka umri wa kustaafu hawakuwa wajinga - "empty vessels". Ni muhimu Rambo akatumia busara zake akajiuzulu maana miaka 63 ni mingi ama akabadili mfumo wa filamu zake. Leo kavunjika shingo, kesho atarajie kutenguka mgongo - ni uzee!
 
 
       Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi