Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Kwanini Watu Wengine Hata Wale Vipi Hawanenepi? Jibu la Kisayansi


Monday, January 04, 2010 2:22 PM
Wakati baadhi ya watu hata wakila kidogo tu vyakula vyenye mafuta huanza kunenepa, kuna wengine hata wale vizuri kiasi gani au wale vyakula vya mafuta kiasi gani huwa hawanenepi hata kidogo, wanasayansi wamepata jibu la suala hilo.
Wanasayansi wamepata jibu la swali “kwanini watu wengine hata wale vipi hawanenepi?” Jibu ni kwamba kama umezaliwa mwili wako ukiwa hauna vimeng’enyo vya mafuta basi wewe hata ule kiasi gani cha vyakula vyenye mafuta mengi kama vile chips, burger na vinginevyo huwezi kunenepa.

Wanasayansi katika chuo kikuu cha California,San Francisco nchini Marekani wamekigindua kimeng’enyo kinachoitwa MGAT2 ambacho ndicho kinachosimamisha jinsi vyakula tunavyokula vinavyonyonywa mwilini.

Kimeng;enyo cha MGAT2 huamua kama mafuta katika vyakula tunavyokula yaingizwe mwilini au yaondolewe mwilini kwa kugeuzwa kuwa eneji.

Kwa maana hiyo kama mwili wako hauna au kiasi kidogo sana cha kimeng’enyo cha MGAT2 basi unaweza ukala chakula chochote unachotaka bila kuhofia kunenepa kwani mafuta yote hayatakuwa yakihafadhiwa mwilini badala yake yatageuzwa eneji.

Katika majiribio waliyofanyiwa panya, wanasayansi waliwachukua panya wa kawaida na panya wa maabara ambao walikuwa hawana MGAT2, walipowalisha milo isiyo na mafuta mengi, panya wote walifanana ukuaji wao.

Lakini walipowalisha vyakula vya Kimarekani vyenye mafuta asilimia 60, panya wa maabara walikuwa na uzito asilimia 40 pungufu ya panya wa kawaida. Pia panya wa maabara miili yao ilionekana kuwa na mafuta asilimia 50 pungufu ya panya wa kawaida.

Panya waliokosa MGAT2 mbali ya kunusurika na tatizo la unene pia waliepukana na maradhi yanayotokana na unene kama vile maini kujaa mafuta.

Wanasayansi wanaendelea na utafiti zaidi ili kugundua dawa za kupunguza MGAT2 ili kuwafanya watu waweze kula vyakula wanavyopenda kwa kiasi chochote kile bila kuhofia kunenepa.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: martin    Monday, January 04, 2010 16:39:34   
 
eneji ndo nini?. au umeshindwa kulitafsiri neno energy kwa kiswahili fasaha??? sema tukusaidie
 
 
Mtoa Maoni: KING    Monday, January 04, 2010 17:12:34   
 
Mmmmmmh kumbeeee! Mi nilikuwa najihisi visivyo ati manake hata nibadili menu vp ngoma vile vile slim kama Snoopy, UBUGUVU kumbe cc sio wagonjwa ni hii MGAT2 ndo inafanya kazi mdau. Ila MOMS016 na KIPARA subirini utafiti zaidi ili kuukwepa unene. Mdau MARTIN kumbe umeelewa? Anyway, KAZI NZURI WANASAYANSI, KILA LA HERI KTK AWAMU ZINAZOFUATA!
 
 
Mtoa Maoni: Dilly    Monday, January 04, 2010 18:27:20   
 
ni vema sana wanasayansi wetu mi nasomea kunguni kwa nini wanakula damu ya watu tu na wasile chakula kingine temu ijayo mtapata majibu kutoka kwa mdau wenu Dilly hapa.

Endeleeni kuniombea nifanikiwe wadau wa NIFAHAMISHE DONTI KAMU

 
 
Mtoa Maoni: Sauali    Monday, January 04, 2010 21:09:06   
 
Huenda hii ikatusaidia pia kujua "Kwanini nchi za kiafrika hata zikiwa na rasilimali kiasi gani hazitajiriki? Ardhi, Jua, Mafuta, Madini, Maji, Milima, hali ya hewa... lakini masikini kama jangwa!
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Wednesday, January 06, 2010 19:12:53   
 
@SAUALI yap!
lkn jibu ni dogo tu! upumbavu bin ubinafsi wa v`zi wetu.
@KING co pekee yetu na MINA na BHAI..

 
 
       Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kweli Mapenzi Hayana Umri...
> Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani
> Maisha Yake Yapo Hatarini Iwapo Atalala
> Utamu na Faida za Tende
> Madada Wanne Wazaa Watoto Wanne Ndani ya Siku Nne
> Babu Aota Mmea wa Njegere Kwenye Mapafu
> Akataa Tsh. Milioni 500 Ili Asiolewe
> Auza Bikira Yake Kwa Tsh. Milioni 500
> 'Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu
> Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza
> Matiti Yapigwa Pasi Ili Kuzuia Watoto Wasibakwe
> Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?
> VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu
> Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake
> Mjadala wa Yai na Kuku Kipi Kilianza Wapata Jibu la Kisayansi
> Nyota wa Filamu za Ngono Anapokuwa Mwalimu wa Sekondari..
> Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130
> VIDEO - Mtoto Azaliwa na Sura Yenye Kinyago China
> Ili Asifariki Analazimika Kula Kila Baada ya Dakika 15
> Afariki Baada ya Kupewa Taarifa ya Kifo Chake
> Watu Wafupi Wako Kwenye Hatari ya Kufa Kwa Magonjwa ya Moyo
> Hatimaye Sio Mungu Tena..
> Baada ya Ajali Mtoto wa Miaka 3 Awa Chapombe na Mvutaji Sigara

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi