|
|
|
VIDEO - Mtoto wa Miaka 7 Mwenye Albamu Tatu za Muziki |

Mtoto Cleopatra Stratan mwenye albamu tatu za muziki |
Saturday, December 26, 2009 5:17 AM
Pamoja na kuwa na umri mdogo wa miaka saba, mtoto Cleopatra Satrana raia wa Moldova anayeishi nchini Romania ameishatoa albamu tatu za muziki, ndiye msanii mdogo kuliko wote kulipwa pesa nyingi na ndiye msanii mdogo kuliko wote duniani kushinda tuzo 3 za muziki za MTV. |
Mtoto Cleopatra Stratan alizaliwa nchini Moldova mwezi oktoba mwaka 2002 na ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa msanii mdogo kuliko wote kupata mafanikio makubwa kwenye biashara ya muziki.
Akiwa na umri wa miaka mitatu, Cleopatra alitoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "La vârsta de trei ani" ambayo aliiuza kwa dola laki tatu ( Takribani Tsh. Milioni 390).
Cleopatra anashikilia rekodi ya kuwa msanii mwenye umri mdogo kufanya shoo ya masaa mawili mbele ya hadhara kubwa ya watu na ndiye msanii mdogo kuliko wote anayelipwa pesa nyingi.
Cleopatra pia anashikilia rekodi ya kuwa msanii mdogo kuliko wote kushinda tuzo tatu za muziki za MTV.
Cleopatra pia ana rekodi nyingine ya kuwa msanii mdogo kuliko wote nyimbo yake kushika namba moja katika chati za muziki duniani. Wimbo wake "Ghita" ulishika namba moja kwenye chati za muziki za Romania na Japan.
Kipaji cha Cleopatra kinatokana na baba yake Pavel Stratan, ambaye ni mwalimu wa muziki.
Wakati Cleopatra baba yake alipokuwa na umri wa miaka mitatu, Baba yake alikuwa akirekodi nyimbo studio wakati Cleopatra akizunguka zunguka ndani ya studio.
Ghafla Cleopatra alichukua maiki na kuanza kuimba nyimbo ya baba yake sambamba naye.
Kila mtu aliyekuwa studio alishangazwa na kipaji cha Cleopatra na huo ndio ukawa mwanzo wa Cleopatra kuingia kwenye biashara ya muziki.
Cleopatra amekuwa akitamba zaidi kwenye nchi za ulaya mashariki akiwa na washabiki wengi sana nchini Romania.
Nyimbo zake zimekuwa zikitafsiriwa katika lugha za kiingereza na kihispania ili ziwafikie watu wa mataifa mbali mbali.
Albamu yake ya pili aliitoa akiwa na umri wa miaka miwili na ilikwenda kwa jina la "La Varsta De 5 Ani" huku nyimbo iliyohiti zaidi ikiwa ni "Zunea Zunea".
Albamu yake ya tatu imetambulishwa nchini Romania wiki hii katika shoo ya nguvu iliyohudhuriwa na mamia ya watu.
Cleopatra amekuwa akitembelea nchi mbali mbali akifanya shoo zake za muziki. Baba yake mbali ya kuwa mpiga gita katika shoo za mwanae pia ndiye meneja wa mtoto huyo mwenye kipaji cha muziki.
Si vibaya kama utaangalia video chini kuona mojawapo ya kazi za msanii huyu mtoto ziliyomfanya atambulike duniani. |
|
|
VIDEO - Mtoto wa Miaka 7 Mwenye Albamu Tatu za Muziki
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Saturday, December 26, 2009 06:16:33
|
|
Mtoa Maoni:
KIPARA
Saturday, December 26, 2009 12:42:49
|
|
Mtoa Maoni:
emma
Saturday, December 26, 2009 13:59:07
|
|
Mtoa Maoni:
Nyoshi
Saturday, December 26, 2009 14:35:07
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Sunday, December 27, 2009 17:20:33
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
More life style news and articles |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|