|
|
|
Mtoto wa Miaka 12 Amzalisha Mama Yake |

Mtoto Courtney akiwa na dada yake mpya Pashia |
Monday, December 21, 2009 7:37 PM
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 amepongezwa kwa ujasiri wake aliouonyesha kwa kugeuka mkunga na kumzalisha mama yake mjamzito mtoto wa kike. |
Mama mmoja wa nchini Uingereza anamshukuru sana mtoto wake wa kiume kwa ushujaa wake wa kutoogopa na kumsaidia katika kujifungua mtoto wa kike nyumbani kwake.
Mtoto huyo, Courtney Senior, mwenye umri wa miaka 12, aligeuka mkunga baada ya mama yake Amanda Creak mwenye umri wa miaka 30 alipozidiwa na uchungu na kuingia leba nyumbani kwake.
Courtney alimuongoza mama yake bafuni kabla ya kuita ambulansi.
Lakini kabla ya ambulansi haijafika, mama yake alianza kujifungua na kumfanya Courtney ajitose kumzalisha mama yake.
Courtney alimuongoza mama yake katika hatua zake zote za kumzaa mtoto wake wa kike na alipomaliza alichukua taulo na kumzungushia dada yake mpya na kumkabidhi mama yake.
"Nilishtuka sana lakini sikuogopa, nilijua kila kitu ninachotakiwa kufanya kwakuwa nilishawahi kuona programu ya uzazi kwenye TV, nilikopi kila kitu nilichokiona kwenye programu hiyo", alisema mtoto Courtney.
Amanda ambaye ni mama wa watoto wanne alikuwa akitarajia kujifungua mtoto wa kike aliyempa jina la Pashia siku ya krismasi.
Lakini bila kutarajia aliingia leba siku ya jumanne wiki iliyopita baada ya kuzidiwa na uchungu wa uzazi.
Mtoto Pashia alizaliwa akiwa na afya njema na uzito wa kilo 2.45.
"Courtney ni shujaa wangu, watoto wengi wa umri wake wangeogopa sana lakini yeye wala hakuonyesha kupaniki", alisema Amanda.
"Atakuwa na uhusiano mkubwa zaidi na dada yake kwakuwa yeye ndiye aliyesaidia kuzalishwa kwake", aliendelea kusema mama huyo.
Kwa ushujaa wake aliouonyesha Courtney alizawadia viatu vipya na mama yake. |
|
|
Source: The Sun
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Mwaego
Monday, December 21, 2009 20:12:36
|
|
Mtoa Maoni:
KIPARA
Monday, December 21, 2009 21:24:05
|
|
Mtoa Maoni:
Bhai.
Monday, December 21, 2009 21:26:22
|
|
Mtoa Maoni:
Dogo salim
Monday, December 21, 2009 21:27:35
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Monday, December 21, 2009 22:02:58
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (10), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
More life style news and articles |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|