Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Ndoa ya Wazazi Wake Beyonce Yavunjika


Mama yake Beyonce, Tina Knowles, na mumewe wa ndoa ya miaka 29 Mathew Knowles.
Sunday, December 20, 2009 1:17 PM
Ndoa ya wazazi wa mwanamuziki nyota wa Marekani, Beyonce, imefikia tamati baada ya miaka 29 ya maisha ya ndoa.
Mama yake Beyonce, Tina Knowles, amefungua madai ya talaka mahakamani kuivunja ndoa yake na mumewe Mathew Knowles iliyodumu miaka 29.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana Tina alifungua jalada la madai ya talaka kwenye mahakama moja ya Texas mwezi uliopita huku tetesi zikisema kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo ni mumewe kutokuwa muaminifu na kuisaliti ndoa yao.

Mathew amekuwa akitajwa sana kwenye vyombo vya habari kwa miaka kadhaa kuwa anatembea nje ya ndoa yake na hivi karibuni alifunguliwa kesi na mwanamke mmoja wa Los Angeles akituhumiwa kumpa mimba na kumtelekeza.

Tina na Mathew walifunga ndoa mwaka 1980 na walizaa watoto wawili Beyonce na Solange. Wana mjukuu mmoja mwenye umri wa miaka 5.

Mathew ndiye meneja wa shughuli za muziki za binti yake Beyonce wakati Tina anasimamia duka lake la nguo linaloitwa "House of Deréon" alilofungua na Beyonce mwaka 2006.

Mwezi juni mwaka huu, jarida moja la udaku la Marekani liliripoti kuwa shughuli za kimuziki na biashara zimewafanya wazazi wake Beyonce waishi mbali mbali kwa muda mrefu.

Beyonce akiongea katika mahojiano na jarida la Giant mwaka jana alisema kuwa amejifunza mengi kutokana na ndoa ya wazazi wake.

Beyonce ambaye alifunga ndoa na rapa milionea Jay-Z mwezi aprili mwaka jana alisema kuwa amejifunza kuwa maisha ya ndoa si lelemama, wazazi wake wamekuwa wakikorofishana na kupatana mara kwa mara na kuna wakati waliishi pamoja wakati mwingine wakiishi tofauti.

Mdogo wake Beyonce, Solange mwenye umri wa miaka 23, aliolewa wakati alipokuwa na umri wa miaka 17 na mchezaji soka Daniel Smith, lakini ndoa yao haikudumu sana na ilivunjika mwaka 2007.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Bhai.    Sunday, December 20, 2009 15:09:56   
 
BUGUVU ii kesi gumu, mimi achia wewe kuwa Judge, sababu wewe iko ishi na ii watu na keo yako iko zungu jua tabia yake na iyo rafiki yake Beyonce.
 
 
Mtoa Maoni: ubuguvu    Sunday, December 20, 2009 15:15:30   
 
wanatafuta majina hawa hawana lolote haya ndiyo matatizo ya shibe wenziwao wanangaika hawajui watakula nini wao wanakesha wafanyi nini ili wandikwe haya tena Bhai na wewe peleka barua ya uchumba kwa watoto wa Obama utandikwa na MOMOS016 mkaliwam na KING watandika comment
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Sunday, December 20, 2009 17:32:31   
 
Tunasema mm na mkubwa wangu NAUTIA K "njia nyepesi ya kumaliza penzi ni ndoa, na njia ya kumaliza ndoa ni kumpenda mwanamke mwengine" haya ndio yaliyotokea kwa hawa wasanii wawili.
Ndo chungu tele zinatawanyika hata hatusikii kitu (km aonavyo UBUGUVU jitu la macommentiz makali!)
BHAI ww iko na muke au iko hpn muke ww?
KING jitahidi usije ukamuacha mkeo na familia yake kwa jumla!
Mdau DeClekers @ MINA nitakupeni kazi ya kunitafutia mchumba mzuri, kinyume cha hapo naingia INDIA kwa BHAI.

 
 
Mtoa Maoni: KIPARA    Sunday, December 20, 2009 22:19:52   
 
huyu mama ni wivu na kasumba za ukomonisti dunia ya leo ni utandawaz na demokrasia lazima kila nchi iwe na sio chini ya vyama 3 sasa na sisi lazima tuende na wakati tuwe na wake 3 kila m"me ili kuondoa matamanio nje ya ndoa huyo mama kama anadai hiyo talaka itakua kosa la jinai maana anakataa mfumo wa vyama vingi utajijuuu utaupinda huooooo
 
 
Mtoa Maoni: KING    Monday, December 21, 2009 08:42:03   
 
Wadau BHAI, UBUGUVU, KIPARA na MOMS016...........mkubwa wetu NAUTIA K majuzi hapa alituachia busara moja juu ya haya ya 'wapendanao' naomba nami niirejee kwa haya ya familia ya Bw. na Bi. Knowles kwamba "wafu kwa wafu wakokotana", MAMBO YA NGOSWE HAYO TUWAACHIE WENYEWE!
 
 
       Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake