|
|
|
Mtoto wa Mwaka Mmoja Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kuogelea |

Mtoto Gibson Walker mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu akiogelea |
Wednesday, December 16, 2009 2:32 AM
Mtoto Gibson Walker wa nchini Australia pamoja na kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu anawashangaza watu wengi kwa uwezo wake wa kuogelea kiasi cha kwamba huwashinda hata baadhi ya watu wazima. |
Mtoto Gibson Walker ana umri wa miezi 18 tu lakini ana uwezo wa kuogelea na kupiga raundi nne katika bwawa la kuogelea lenye urefu wa mita 25.
Akifanya mazoezi katika kituo cha mazoezi ya kuogelea cha Gulliver Coomera Swim Centre, Gibson huogelea kwa mwendo kobe wa taratibu lakini hufanikiwa kumaliza raundi nne kuzunguka bwawa la kuogelea bila kupumzika.
Baba yake Gibson, Mark alisema kuwa alianza kumfundisha mwanae kuogelea tangia alipokuwa na umri wa miezi sita na ghafla alianza kupenda kuogelea.
"Anajiamini sana anapoogelea kiasi cha kunifanya nisiwe na hofu yoyote", alisema baba wa mtoto huyo.
Mafunzo ya kuogelea aliyopewa akiwa na umri mdogo yalimsaidia mtoto huyo kuokoa maisha yake wakati alipodondoka pembeni ya bwawa la kuogelea na kuangukia kichwa kabla ya kuangukia kwenye bwawa la kogelea.
Gibson badala ya kuanza kulia kama watoto wenzake ambavyo wangefanya, aliogelea hadi kwenye ukingo wa bwawa hilo na kujitoa mwenyewe nje ya bwawa hilo ndipo akaanza kulia.
Mwalimu wake wa kuogelea Terry Gulliver ana rekodi nzuri ya kuwafundisha watoto wenye umri mdogo kuogelea. Aliwahi kumfundisha mtoto wa miaka mitatu kuweza kuogelea mita 1500 bila matatizo yoyote.
"Kuogelea ni mchezo muhimu sana kwa maisha yetu", alisema Gulliver.
"Idadi ya watu wanaofariki kwa kuzama katika maji ingepungua kama watoto wote wangefundishwa kuogelea angalau mita chache", alimalizia kusema mwalimu huyo wa kuogelea. |
|
|
Source: News Agencies
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Wednesday, December 16, 2009 09:17:53
|
|
Mtoa Maoni:
KING
Wednesday, December 16, 2009 09:38:47
|
|
Mtoa Maoni:
DeClarkes
Wednesday, December 16, 2009 10:21:35
|
|
Mtoa Maoni:
mkaliwam
Wednesday, December 16, 2009 10:22:13
|
|
Mtoa Maoni:
kadudu
Wednesday, December 16, 2009 14:57:04
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (10), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
More life style news and articles |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|