|
|
|
Mtoto wa Miaka 6 Mwenye Uwezo wa Kuvuta Magari |

Mtoto Santhosperumal akionyesha uwezo wake wa kuvivuta vitu vyenye uzito mkubwa |
Monday, December 14, 2009 10:03 PM
Pamoja na kuwa na umri wa miaka 6 tu, mtoto huyu wa nchini Malaysia amewashangaza watu wengi kwa uwezo wake wa kulivuta gari lenye uzito wa tani mbili. |
Mtoto T. Santhosperumal wa mji wa Klang nchini Malaysia amejipatia umaarufu mkubwa kwa uwezo wake wa kuvivuta vitu vyenye uzito mkubwa ambavyo hata baadhi ya watu wazima wasingeweza hata kuvisogeza achilia mbali kuvivuta kwa mita kadhaa.
Akitumia mkanda uliofungwa kiunoni mwake, mtoto huyo alifanikiwa kulivuta gari lenye uzito wa tani 1.650 mbele ya mamia ya watu waliojazana kushuhudia uwezo wake.
Baba wa mtoto huyo, N. Thiagu, alijivunia uwezo wa mtoto wake na alisema kuwa anaamini siku moja mtoto wake atavunja rekodi ya dunia.
"Santhosperumal, ana uwezo wa kufanya kila kitu anachotaka kufanya au kujifunza, alipokuwa na umri wa miaka minne alianza kuendesha gari hivi sasa anaweza kuendesha hata malori", alisema baba wa mtoto huyo.
Mama wa mtoto huyo naye alijivunia maguvu ya mwanae na kuongeza kuwa mtoto wake anakula chakula sawa na watoto wengine hamna lishe maalumu anayopewa.
Santhosperumal anapenda kuangalia katuni kama watoto wengine isipokuwa katuni anazozipendelea zaidi ni zile zinazoonyesha matumizi ya nguvu katika shughuli mbali mbali.
"Siku moja nitawaonyesha watu uwezo wangu kwa kuivuta ndege", alitamba mtoto huyo. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Monday, December 14, 2009 22:35:31
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Tuesday, December 15, 2009 01:11:23
|
|
Mtoa Maoni:
soud
Tuesday, December 15, 2009 03:35:45
|
|
Mtoa Maoni:
DeClarkes
Tuesday, December 15, 2009 10:24:40
|
|
Mtoa Maoni:
SONGA SONGA
Tuesday, December 15, 2009 11:14:00
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
More life style news and articles |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|