|
|
|
VIDEO - Bibi wa Miaka 75 Awa Bingwa wa Kudansi |

Bibi Jones akionyesha manjonjo yake katika mashindano ya kudansi |
Saturday, December 12, 2009 12:51 AM
Umri haukuwa kikwazo kwa bibi wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 75 ambaye kutokana na uwezo wake mkubwa wa kudansi aliwafunika vijana wote wa Hispania na kutwaa taji la ubingwa wa kudansi nchini humo. |
Paddy Jones, bibi wa kiingereza anayeishi nchini Hispania alianza kupenda kudansi miaka mitano iliyopita baada ya mumewe kufariki, yaliripoti magazeti ya Uingereza.
Bibi Jones alikuwa mmoja wa washiriki wa mashindano makubwa ya kutafuta watu wenye vipaji nchini Hispania yanayokwenda kwa jina la Tu Si Que Vales.
Katika mashindano hayo makubwa yanayorushwa live na televisheni moja kubwa nchini Hispania, Bibi Jones alidansi pamoja na patna wake wa kiume mwenye umri wa miaka 35.
Bibi Jones aliwashangaza majaji na watu walioshuhudia Live mashindano hayo kwa miondoko yake ya dansi ambayo bila shaka vijana wengi hawawezi kuifanya. Aliweza kujizungusha kwa spidi huku akijirusha juu na kupita katikati ya miguu ya patna wake.
"Najiona mwenye bahati sana, naweza kudansi kama hivi, nafikiri itanibidi niendelee kudansi kwa miaka michache ijayo", alisema bibi Jones.
Chini ni VIDEO inayoonyesha jinsi Bibi Jones alivyolitwaa taji la kudansi. |
|
|
VIDEO - Bibi wa Miaka 75 Awa Bingwa wa Kudansi
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Mchafukoge
Saturday, December 12, 2009 02:41:11
|
|
Mtoa Maoni:
mdau
Saturday, December 12, 2009 05:30:49
|
|
Mtoa Maoni:
Bhai
Saturday, December 12, 2009 09:57:31
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Saturday, December 12, 2009 10:11:19
|
|
Mtoa Maoni:
DeClarkes
Saturday, December 12, 2009 12:23:27
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (8), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za burudani |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|