|
|
|
Familia Inayoongea na Watu Waliofariki |

Kylie na watoto wake wanaodaiwa kuwaona mizimu na kuzungumza na watu waliokufa |
Saturday, December 05, 2009 3:02 PM
Familia hii ya nchini Uingereza inadai kuwa na uwezo mkubwa wa kuwaona malaika, mizimu na kuzungumza na watu waliokufa. |
Kylie Holmes, mama wa watoto watatu anadai kuwa na uwezo wa kuwaona malaika wakati watoto wake Jade mwenye umri wa miaka 11, Amba mwenye umri wa miaka 9 na Leo mwenye umri wa miaka 5 wanadaiwa kuwa na uwezo wa kuzungumza na kuona vitu ambavyo watu wengine hawavioni wala hawavisikii.
Mtoto Jade yeye ana uwezo wa kukumbuka matukio yaliyopita, Amba ana uwezo wa kuyaona mizimu wakati Leo anadaiwa kuwa na uwezo wa kuongea na watu waliokufa.
"Wamekuwa wakiona na kusikia vitu ambavyo wengine hawavioni wala kuvisikia, Hali hii imekuwa ikitokea katika maisha yao ya kila siku", alisema mama wa watoto hao alipokuwa akiongea na gazeti la The Sun la Uingereza.
Kylie anasema kuwa yeye na watoto wao wamekuwa wakitembelewa na mamia ya watu kila siku wanaotaka kuzungumza na ndugu zao waliokufa na watu wengine wanaotaka kutibiwa matatizo yao.
Mtoto wake mmoja huchora michoro ya ajabu ajabu isiyoeleweka akielezea matukio yaliyopita na yajayo.
Kylie alisema kuwa alianza kuwaona malaika alipokuwa na umri wa miaka 20 baada ya kulazwa hospitali alipomeza dozi kubwa ya dawa kufuatia stress za matatizo katika mahusiano yake ya kimapenzi.
Kylie anasisitiza kuwa alipoamka hospitalini aliona mwanga ulio kwenye umbile la mtu ambao ulimwambia kuwa atapona.
Anasema kuwa alipopona na kurudi nyumbani kwake alishangaa kukuta chumba chake kimepambwa na manyoya meupe ya ndege na malaika aliyemuona hospitali alimtokea tena.
Kylie anadai kuwa tangia siku hiyo amekuwa akiwasiliana na malaika wake ambaye amekuwa akimsaidia kuyatatua matatizo ya watu wanaofika nyumbani kwake.
Hata hivyo mume wa Kylie, Bw. Eic ambaye ni mwanajeshi mstaafu ambaye pia ndiye baba wa watoto hao haamini kuwa mkewe na watoto wake wana uwezo wanaodai kuwa nao.
"Hawafanyi kitendo chochote cha kumdhuru mtu .. lakini mimi siamini hata kidogo wanachokisema", alisema Eric. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
ubuguvu
Saturday, December 05, 2009 17:31:07
|
|
Mtoa Maoni:
dayame 2005
Saturday, December 05, 2009 19:42:35
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Saturday, December 05, 2009 19:45:02
|
|
Mtoa Maoni:
Ntarambe
Saturday, December 05, 2009 21:55:30
|
|
Mtoa Maoni:
muyomba
Saturday, December 05, 2009 23:03:42
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
More life style news and articles |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|