Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mrisho Mpoto Aanzisha Bendi Yake inayoitwa 'Mjomba'


Mrisho Mpoto
Friday, November 27, 2009 11:52 PM
Mwamamuziki nyota wa kugh'ani Mrisho Mpoto ameanzisha bendi yake ijulikanayo kwa jina la Mjomba bendi na kuwaahidi washabiki wake kuwa bendi hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali.
Akizungumza na Nifahamishe katika mahojiano maalumu yaliyofanyika katika hoteli ya Ubungo Plazza alisema nia ya kuanzisha bendi hiyo ni kutaka kukidhi matakwa ya wapenzi wake.

Mjomba bendi inaundwa na wanamuziki kumi ambao wametoka sehemu mbalimbali na kuamua kuunda kundi hilo ambalo kiongozi mkuu ni Mpoto.

Kiongozi mwimbaji Ismail Shabani (kapila) alisema kuwa bendi hiyo imeundwa mwaka huu na bado hawajapata sehemu ya kupigia ila kwa sasa wanafanya mazoezi katika ukumbi uliopo Mbezi Tangi Bovu.

Mpoto aliwataja waimbaji waliopo kwenye bendi hiyo kuwa ni mshiriki wa shindano la kutafuta vipaji (BSS) ambaye alifika katika kumi bora na kutolewa katika nafasi ya sita bora Merry Lucos, Abuu mwana wa Zanzibar na Esmail Kipila.

Wengine ambao wanaunda kundi hilo wakiwa katika nafasi mabalimbali aliwataja kuwa ni pamoja na Nuruce, Bcb, Sija, Mlanda, Mbwana Mponda, Joji Choka, Peter na Choyoha.

Tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo kumekuwa na manufaa makubwa kutokana na bendi hiyo kupata mialiko mingi ya kiserikali kwenda kutumbuiza katika shughuli mbalimbali za kiserikali.

Kiongozi huyo wa waimbaji alisema bendi hiyo imekuja kuleta burudani kwa wananchi hasa wale wapenda muziki wa dansi na kutabainisha kuwa bendi hiyo ina kila kitu ikiwemo michezo ya maigizo.

Bendi imeanza vizuri sana tofauti na tulivyofikiria mwanzoni na hii imetokana na baadhi ya watu hasa wanamuziki wakongwe kutueleza kuwa tuanzishe bendi tuwe tunapiga live siyo kukopi, alisema Ismail.

Kwa upande wake alipoulizwa kiongozi huyo kuhusiana na soko la muziki hapa nchini alisema kuwa wao wamejipanga vizuri kibiashara na kutoa burudani kwa ujumla alipoulizwa ni bendi gani ambayo anaipenda alisema hakuna bendi zaidi ya Msondo ngoma.

Mrisho Mpoto amejipatia umarufu mkubwa hapa nchini kutokana na aina ya muziki wake anaoupiga.

Kwa kipindi hiki amekuwa akivuma na wimbo wake ambao umempa umarufu wa "Mjomba nikipata nauli nitarudi".

Mjomba hakupenda kutaja umri wake ila alisema kuwa yeye ni baba wa watoto wawili wote wa kiume ambao aliwataja kuwa wa kwanza anaitwa Manjo na wa pili anaitwa Mrisho.

 
Na Kaimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: DeClarkes    Saturday, November 28, 2009 11:37:55   
 
Kila siku najiuliza ni mtindo gani ama ni jinsi gani muziki wa Mrisho Mpoto unavyochezeka sijui? Labda watu wanisaidie, naona ngonjera si ngonjera mashairi sijui ni rap?? Anyway, Mrisho hongera kwa kuanzisha bendi lakini nadhani ningekushauri uanzishe na kwaya maana muziki wako tunachopenda ni tenzi zako na sio beats. Hauchezeki hata ukimwuliza Nipa!
 
 
Mtoa Maoni: mtenya kitwana    Wednesday, March 17, 2010 14:46:43   
 
mjomba ka kibwaya tucheze ngoma ,safariri ndefu inataka uvumilivu,na maisha mbio za vijiti,kwa iyo kaza buti mjomba.
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake