Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Blandina - Autosa Unesi Awe Msanii wa Maigizo


Thursday, November 26, 2009 2:54 AM
KUNa umuhimu mkubwa wa wazazi nchini kuchunguza vipaji vya watoto wao kabla ya kuwapangia nini cha kufanya hasa katika suala zima la masomo. Mfano mzuri ni mwanadada Radhia Hassan Mtetemela ambaye aliacha kazi yake ya unesi kuwa msanii wa maigizo.
Suala hili halina budi kupewa uzito kwa sasa, kutokana na ukweli kuwa vijana wengi wanapelekwa kujifunza fani ambazo si zao huku vipaji vyao vikiachwa vinateketea.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mwanadada Radhia Hassan Mtetemela. Mara baada ya kumaliza elimu yake ya Msingi katika shule ya Mwananyamala Kisiwani mwaka 2000, Radhia aliyezaliwa mwaka 1984 Morogoro vijijini, alipelekwa kusomea mafunzo ya Unesi.

Radhia anaweka bayana kuwa mafunzo hayo ya unesi aliyapata katika chuo cha Msimbazi Centre kilichopo Ilala jijini Da es Salaam mwaka 2006 na mafunzo yake ya vitendo aliyafanya katika hospitali ya Burhan iliyopo Posta jijini Dar es Salaam mwaka 2007.

Lakini pamoja na kupata mafunzo hayo ya unesi, bado Radhia hakuwa na shauku ya kufanya kazi hiyo kutokana na fani hiyo kutokuwa ndani ya damu yake. “Sikupenda kuwa nesi, kwa hiyo sikuendelea na kazi hiyo” anasema msanii huyo.

Baada ya kuachana na kazi hiyo, alikwenda kusomea mambo ya mapambo katika chuo cha ufundi stadi (VETA) kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Kama ilivyokuwa kwenye unesi, hata baada ya kuhitimu mafunzo hayo, hakuendelea na fani hiyo. “Bado kuna kitu kilikuwa kimenikaa ndani ya kichwa changu na niliona ndicho ninachostahili kufanya katika maisha yangu,” anasema Radhia.

Je ni kitu gani hicho?. Binti huyo mwenye umbo la kuvutia anaweka bayana kuwa sanaa hasa sanaa ya maigizo ndiyo iliyokuwa imemtawala kichwani mwake.

Tangu nilipokuwa mdogo nilipenda sanaa na nilijihisi kuwa nina kipaji cha kuigiza, kwa hiyo kila nililolifanya niliona kama napoteza tu wakati, lakini huku ndiko kwenyewe,” anasema msanii huyo.

Kutokana na hali hiyo, mwaka 2006 alianza kampeni zake za chinichini za kufanya sanaa kwa kujiunga na vikundi mbalimbali vya sanaa maeneo ya nyumbani kwao Mwananyamala.

“Kwa kuwa nilikuwa napenda sanaa lakini sijawahi kuifanya, ilinibidi nianze kwenye msingi, yaani kujifunza kwa kujiunga na vikundi mbalimbali kwa lengo la kupata uzoefu,” anasema msanii huyo.

Mwaka 2008 aliangukia katika mikono ya msanii mkongwe na mahiri hapa nchini, Mohamed Jengua ‘Mzee Jengua’ katika kundi lake la Kidedea lenye maskani yake Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alikaa na kundi hilo kwa muda wa mwaka mmoja lakini hakuweza kupata bahati ya kushiriki katika michezo yoyote ya kuigiza iliyotolewa na kundi hilo.

Kwa kuwa alikuwa na kiu ya kusaka mafanikio, mapema mwaka huu alijiengua katika kundi hilo na kujiunga na kundi la Amka Sanaa Group ambalo lilikuwa linaonyesha michezo yake katika kituo cha ITV.

Hata hivyo pamoja na kujiunga na kundi hilo, bado hakuweza kupewa nafasi kubwa ya kushiriki katika michezo iliyokuwa inatolewa na kundi hilo.

“Nikiwa na kundi hili tulitoa michezo zaidi ya miwili pale ITV, lakini sikuweza kupata nafasi, labda waliona kuwa sina uwezo wa kuigiza”

Lakini wahenga walisema mgaa gaa na upwa hali wali mkavu, na riziki ya mtu siku zote iko mikononi mwa mtu, kwani wakati Amka walikuwa hawamfikirii, milango aya mafanikio ikafunguka kwa upande mwingine.

“Nakumbuka siku moja nilikuwa niko mazoezini, kuna msanii mwenzetu anaitwa Omari alinieleza kuwa kuna rafiki yake anaitwa Seleman Mkangara anatafuta msanii wa kucheza katika filamu yake Blandina, hivyo kama sitojali anipeleke nikafanye majaribio.

“Kwa kweli nilishtuka niliposikia jina la Mkangara kwani huyu ni miongoni mwa waandaa filamu ambao ninawaheshimu. Kwa hiyo niliona nafasi yangu kwake ni ndogo, lakini Omari alinishawishi na kunisihi kuwa nikajaribu bahati yangu naweza kufanikiwa.

Msanii huyo anasema kuwa alipofika aliwekwa mbele ya kamera na kuanza kufanyiwa majaribio huku akiwa na hofu, lakini Mkangara alijaribu kumtoa hofu na kumfanya awe huru.

“Nilikuwa naogopa kutokana na watu wote walio mbele yangu ni wageni, lakini Mkangara alinitoa hufu na kunifanyia mambo ambayo yaliniondoa hofu na kufanya vyema.

Mara baada ya kumaliza alinieleza kuwa atanipigia simu kwani tulikuwa wengi tuliofanya majaribio kuwania nafasi hii. Baada ya siku mbili alinipigia simu na kunieleza kuwa nimepita, kwa kweli nilifurahi sana, kwani niliona sasa naanza kupata mwanga,”.

Msanii huyo anasema kuwa mara baada ya kusaini mkataba, alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu hasa baada ya kupewa muongozo (script) ya filamu hiyo ya Blandina.

“Kwa kweli Blandina ni filamu ngumu kuicheza kwani inavitu vingi vinavyohitaji uhalisia na hisia za hali ya juu. Lakini nimefarijika kuona kuwa nimeicheza vizuri, nimejifunza mengi kupitia filamu hii,” anasema msanii huyo.

Radhia anasema kuwa anamshukuru sana Mkangara, kwani mbali ya kugundua kipaji chake, lakini ameweza kumjenga sana kisanii.

“Utakapoangalia filamu hii utaona nimecheza kwa kiwango cha hali ya juu, lakini ukweli nimetengenezwa na Mkangara na kwa kufanikiwa kuicheza filamu hii naona milango ya mafanikio kwangu sasa iko wazi".

 
Na Kaimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Ubuguvu    Thursday, November 26, 2009 11:10:38   
 
Kwanza nakupongeza kwa kupata unacho kitaka na kufanya kazi unayoipenda hongela kwa hilo pili tumeambiwa alijiunga na msanii mkongwe M. Jengua ktk kundi lak lenye maskani yake kinondoni mimi nauliza maskani yapo chini ya mti sababu jengua anaishi kwa mama yake baada banda lake kuvunjika paa tatu mzee S. Mkangara akitaka kufanya kama jay-z na Rihanna huu ndiyo wakati wake ukimkosa hapa jina likikua ndiyo basi ila mimi si mkushauri wala sikuungi mkono kufanya hivyo. nne mimi sio huyu mwanamke kama amefanya accomplishment kwa ekti hiyo filam ila na kubaliana Kaimanzila huyu mtoto mrembo KING ukimuona utammezea mate
 
 
Mtoa Maoni: DeClarkes    Thursday, November 26, 2009 11:14:49   
 
Hongera dada yangu kwa kutaka kile kitu ambacho unakiweza. Sijui kama unesi uliosomea ungekutoa zaidi ya kuliwa na madaktari wakware ambao hutuambia tusifanye ngono lakini wenyewe wakali kwa kula wake za watu (Kama kajamaa kanachomla Nipa). Mimi ni Mhasibu huku Zenji, lakini sijui lakini kama kweli Msimbazi kuna chuo cha manesi?
 
 
Mtoa Maoni: kipara    Thursday, November 26, 2009 20:26:03   
 
pole sana anty kuwa muigizaji filamu bongo sawa na kutia mkono gizani cd zako kesho zina chapishwa vichochoroni huto pata hata nusu ya gharama bora ulivyo kuwa nursi ukaambulia posho na rushwa
 
 
Mtoa Maoni: msema wazi    Friday, November 27, 2009 02:16:17   
 
msowea punfa hapandi farasi mmungu kamuumba na kichwa kasoma somo gumu kafaulu baad ya kutafuta kazi spital za private akatuliza ball kaona bora akahaingike na filam haya tuyaoneee wanafata umaaarufu tu
 
 
Mtoa Maoni: KING    Friday, November 27, 2009 09:08:11   
 
Dah! Hakika Bi. Radhia mlimbwende kweli, enzi zetu mtoto kama huyu UBUGUVU tulikuwa tunamwita 'kipusa'. Anyway, kwa hakika mchagua njia ndiye ajuaye inapoelekea...........WACHA TUHESHIMU CHAGUO LAKE MAANA NI MAISHA YAKE BINAFSI!
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi