Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Busta Rhymes Kuinogesha Fiesta Jioni Hii


Busta Rhymes
Saturday, November 21, 2009 5:39 PM
MKALI wa muziki wa hip hop, Busta Rhymes anatarajiwa kutumbuiza jioni hii kwenye tamasha la Fiesta One Love linalofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Posta jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo ambalo tayari limeshaanza, na kuandaliwa na Clouds FM linafanyika kwa mara ya 10 na linashirikisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Ruge Mutahaba amesema Rhymes ametua nchi akiwa na kundi lake lenye wasanii tisa tayari kwa kuwapa burudani mashabiki.

Tamasha hilo linafanyika kwenye viwanja vya kilichokuwa Chuo cha Kampuni ya Simu Tanzania, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Mutahaba alisema nyota wa hip hop atatumbuiza kwa muda wa saa moja na nusu bila mapumziko lengo ni kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wake na kwamba mwaka huu tamasha hilo litakuwa la aina yake.

Alisema litakuwa majukwaa matatu ambayo yote yatakuwa bize na hakutakuwa na muda wa kupumzika kwa wasanii.

"Rhymes ni msanii mahiri ambaye amewahi kupata tuzo mbalimbali za billboard, ni msanii anayebadilika kulingana na mazingira anakubalika kwa vijana na wazee,"alisema mratibu huyo.

Baadhi ya nyimbo ambazo anatamba nazo msanii huyo ni pamoja na Arab money, Turn it Up, Woo Hah, Make it Clap ambao kamshirikisha Spliff Star, Hey Ladies, I ever saw on.

Msanii huyo wa kimataifa atashirikiana na wasanii wa wazawa wakiwamo Ali Kiba, Marlow, Barnabas, Daz Nundaz, Bushoke, TMK Famili, Juma Nature na Wanaume Halisi, Profesa Jay, Belenine, Hussein Machozi, Lady Jaydee na Ray C

 
Ismail Ally    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Ubuguvu    Saturday, November 21, 2009 18:57:57   
 
Basi hapo wabongo watajaa hapana hata pakueka mguu na serekali iyangalie mikusanyinko isiokua na umuhimu wakati huu dunia inakabiliwa na janga la mafua ya ngurue mkusanyiko kama huo ni hatari virusi vinavyo sababisha ugonjwa huo kitaalamu vinaitwa n1h1 vinasamba haraka sana sasa tz musijifanye nyinyi munaishi ktk dunia nyengine nchi nyingi zinazuia mkusanyiko waina yoyote usiokua na lazima. Ismail hiyo nyimbo ya woo hah ya kingeleza au kichina. Bhai 2likumic sn hapa MOMS016 ndiyo anafahamu nimemwambia nini Bhai
 
 
Mtoa Maoni: KING    Saturday, November 21, 2009 19:18:20   
 
RUSUMO.COM pamoja mdau ktk kulisongesha............UBUGUVU eeeeeee wacha ndugu zako nasi walau tukatoe ukungu machoni na kupata picha za ukumbusho. Nimevutiwa na ujumbe wa hawa waandaaji manake hakika hii dunia yahitaji ONE LOVE na c vinginevyo! MOMS016 vp mdau nawe unaogopa mafua ya "haram"?
 
 
Mtoa Maoni: kipara    Saturday, November 21, 2009 20:02:07   
 
@MDAU RUSUMO.COM wewe ni mwisho wa reli juzii niliiweka likizo ipod yangu huna kitu kibaya kwa fani zote hongera mdau mmungu akupe moyo wa jabali uyastamilie yote yanayokukera .amin. busta wafurahishe wakina king..moms016..baada ya kiza na kabla ya mafuriko ONE WORLD ONE LOVE
 
 
Mtoa Maoni: solo    Saturday, November 21, 2009 21:20:58   
 
wewe ubuguvu ni mtu mwenye choyo,mafua ya ndege hayo kwa sababu ya mkusanyiko wa kuumuona mtu maarufu tu,bongo hakuna mafua ya ndege huku watu wamekufa lakini wa hai malaria kama kula kuku kwa mrija,mafua ya ndege kwa wazungu tu,
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Saturday, November 21, 2009 21:52:06   
 
Mdau KING, UBUGUVU keshanitisha kuna maradhi ya H1N1 sasa naona nikae pembeni manake tutaambukizana na matibabu yenyewe mpaka upande ndege..
KIPARA umeongea cha maana sana, kutakuwa na mishumaa au viba..?
Na hao kina Juma Nature/Bushoke /TMK si wakaimbe "barua" "Dar mpk Moro" marekani??? Au hakuna viza?
UBU nyimbo ya Woo Hay ni ya kihindi, muulize BHAI.

 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi