Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
'Natamani kuwa mwimbaji mahiri' - Aaliyah


Mnenguaji mahiri wa FM Academia , Aaliyah Moses
Tuesday, November 03, 2009 7:25 AM
Miongoni mwa wanenguaji mahiri wa muziki wa dansi nchini Aaliyah Moses ambaye amekuwa akinengua kwa miaka 11 sasa, amesema kuwa wakati wake umefika wa kuachana na unenguaji na kuwa mwimbaji mahiri nchini.
UNAPOZUNGUMZIA muziki wa dansi nchini hasa katika suala zima la taaluma ya unenguaji, utakuwa umefanya kosa kubwa kama kwenye mazungumzo yako hutomzungumzia Aaliyah Moses.

Mnenguaji huyu ambaye kwa sasa yuko na bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', ni miongoni mwa wanenguaji mahiri na waliodumu katika fani hiyo kwa miaka mingi ambapo amekuwa mnenguaji kwa miaka 11 sasa.

Mwadada huyo alianza fani akiwa na umri mdogo mwaka 1998 katika kundi la Billbams lililokuwa linatumbuiza katika ukumbi wa Bilicanas jijini Dar es Salaam akiwa na vijana wenzake kama Hassan Nyemwela 'Super Nyamwela', Aisha Madinda na Omari Bokilo.

Lakini kwa sasa mwanadada huyo anataka kupiga hatua zaidi nayo si ingine bali kutoka kunengua huku akisindikizwa na sauti za waimbaji mbalimbali, na kuwa mmoja wa waimbaji mahiri na sauti yake ikiwa inawaongoza wanenguaji.

"Nimenengua kwa muda mrefu, nadhani sasa nahitaji kupiga hatua zaidi kutoka hapa nilipo. Nahitaji kuwa miongoni mwa waimbaji mahiri," anasema Aaliyah.

Jitihada za mwanadada huyo kutimiza malengo yake zimeanza kuonekana, kwani hivi sasa ameanza kushiriki kuimba nyimbo mbalimbali katika maonyesho ya bendi yake ya FM Academia.

"Nimeanza kuimba kidogo kidogo, naamini baada ya muda fulani nitakuwa muimbaji mahiri wa kike hapa nchini," anasema mwanadada huyo machachari awapo ndani ya jukwaa.

Ni sababu gani hasa zilizomfanya mwanadada huyo kutaka kuwa mwimbaji?.

Muziki uko kwenye damu yangu na muziki ndiyo maisha yangu. Nadhani hicho ndicho kinachonipa msukumo zaidi wa mimi kujifunza kuimba," anasema mnenguaji huyo.

Aaliyah anasema kuwa yeye anaamini kuwa atakuwa kwenye muziki katika kipindi cha maisha yake yote, lakini hawezi kuendelea kuwa katika muziki kwa kuwa mnenguaji.

"Umri unazidi kwenda. Naamini kabisa itafika wakati sitoweza tena kunengua. Itanilazimu kuachana na fani hiyo, lakini kama nikiwa mwimbaji nitaendelea kuwemo kwani uimbaji hauna umri," anasema.

Mwanadada huyo mwenye mtoto mmoja, alianza fani ya unenguaji mwaka 1998 kwenye kundi la Bilbams lililokuwa likifanya maonyesho yake katika ukumbi wa Bilicanas, akiwa na watoto wenzake kama Aisha Mohamed 'Aisha Madinda', Hassan Nyamwela 'Super Nyamwela' na Omari Bokilo.

Mwaka 2000 alijiunga na bendi ya The Millenium iliyokuwa ikiongozwa na Maroston Patcheko na mwaka 20001 alichukuliwa na mwanamuziki Kanda Bongoman kutoka Kongo na kufanya naye ziara ya kuzunguka bara la Afrika.

Mwaka 2002 alirejea nchini na kuchukuliwa na kampuni ya African Stars Entertainment (ASET) na kuzitumikia kwa nyakati tofauti bendi zinazomilikiwa na kampuni hiyo, African Stars 'Twanga Pepeta' na African Revolution 'Tam Tam'.
Pia kwa nyakati tofauti amekuwa akienda Omani kufanya maonyesho.

Mwaka 2004 alijiunga na bendi ya Mchinga Sound iliyokuwa ikiongozwa na Ali Choki ambaye kwa sasa ni kiongozi wa Extra Bongo.

 
Na Kaimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Bhai.    Tuesday, November 03, 2009 08:38:24   
 
Fikira zuri sana taka jua imba, ii kazi neguanegua taka tandani bas, pana onesa watu migine.
 
 
Mtoa Maoni: KING    Tuesday, November 03, 2009 08:54:00   
 
Daima kuwa na malengo ya juu zaidi ni jambo bora zaidi. KILA LA HERI DADA!
 
 
Mtoa Maoni: Ubuguvu    Tuesday, November 03, 2009 16:36:35   
 
Kabla hujawa mwanamuzi mkubwa kwanza uwe mwanamuziki sasa wewe mnenguaji tu sawa na biza ktk mchuzi na kwa mujibu nilivyo snma hii habari nimefahamu kwa hana anacho kijua ktk mziki na wala hawa kipaji na hakutengeneza kipaji ili awe muimbaji bali kamua sasa awe muimbaje eti kwa sababu tu kaona anazeeka zeeka sasa vijana wadogo wanampiga bao na hapo baadae hatoweza tena kunengua ndiyo anatafuta njia ya kulida sembe ndiyo anataka kua muimbaji, samahani Kaimanzila dont misunderstand naona mwenyewe umemfagili sana
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi