Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Ferre Gola kutua Bongo mwezi ujao


MWANAMUZIKI mahiri wa Kongo, Ferre Gola Bataringe
Thursday, October 22, 2009 4:58 PM
MWANAMUZIKI mahiri wa Kongo, Ferre Gola Bataringe anatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao kwa onyesho moja la muziki litakalofanyika mjini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Udhamini na Matukio wa kampuni ya New Habari (2006) Limited, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam mapema leo kwamba mwanamuziki huyo ataambatana na kundi la wanamuziki 17.

"Ferre atakuwepo hapa mwezi ujao kwa onyesho moja la muziki baada ya hapo atakwenda Burundi na Rwanda kwa ajili ya onyesho moja moja katika nchi hizo," alisema.

Mwendapole alisema maonyesho ya Rwanda na Burundi yatakuwa maalum kwa ajili ya kuzindua uuzaji wa tiketi za bahati nasibu ya shindano la Miss East Africa.

Katika msafara huo pia watakuwepo wanenguaji wa kike watano ambao ni Sabena wa Kayembe, Vick Moleka, Nancy Mbemba, Renate Kunga na Patricia Isako.

"Kuhusu tarehe ya onyesho na wapi onyesho litafanyika, tutatangaza siku ambayo tunatangaza mdhamini mkuu wa onyesho hili ambalo ni la kwanza Ferre kufanya peke yake Tanzania hii pia ni ziara ya kwanza kwa Ferre kwa Afrika Mashariki tangu ajitoe Quarter Latin Internationale ya Koffi Olomide," alisema.

Kabla ya kuanzisha bendi yake, Ferre aliwahi kupigia bendi ya Wenge Musica BCGB ambapo alikuja nayo nchini mwaka 1997, baadaye akabaki na bendi ya Wenge Maison Merre ya Werrason iliyomeguka kutoka BCBG na akatembelea tena mwaka 2000.

Ferre alijiondoa katika bendi hiyo ya Werrason na kuanzisha Le Marquizer de Maison Merre akiwa na repa Bill Caludji Clinton na Baby Ndombe, kabla ya kuchukuliwa na Koffi Olomide.

Kwa sasa anatamba na albamu zake Sens Interdit, Lubukulumu na Queist Derrierur Toi yaani nani yuko nyuma yako ambayo ni albamu yake mpya.

 
Ismail Ally    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: KING    Friday, October 23, 2009 10:21:23   
 
Wadau wa burudani za kikongo, chukueni hii.......mi Bongo fleva bwana! Ok, karibu Tz Ferre Gola Bataringe. Natumai hutawaangusha 'wadau' wako.
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake