Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Aurora Yajitosa Miss Utalii Ilala 2009


Baadhi ya warembo wa Miss Utalii, 2009
Tuesday, October 20, 2009 4:53 PM
KAMPUNI ya Aurora Security imetoa sh mil. 25 kwa waandaaji wa shindano la kumsaka Miss Utalii Ilala 2009 ili kufanikisha shindano hilo.
Fedha hizo zinajumuisha usafiri, chakula kwa warembo wakati wa kambi, pamoja na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Huu utakuwa muendelezo wa kampuni hiyo katika kusaidia kufanikisha mashindano ya Miss Utalii ambapo hivi karibuni ilidhamini shindano la Miss Utalii Temeke lililofanyika katika Ukumbi wa City Garden.

Kwa mujibu wa mratibu wa Miss Utalii Ilala, Amina Boke, shindano hilo linatarajiwa kufanyika Novemba 6 mwaka huu katika ukumbi wa Dar West Park uliopo Tabata, jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Aurora Security, Ally Aurora, alisema kuwa wameamua kuendelea kusaidia Miss Utalii kutokana na kugundua ubora na umuhimu wa shindano hilo kwa Tanzania kwani linalenga kuitangaza Tanzania kupitia utalii na rasilimali zilizomo nchini ikiwa ni pamoja na vivutio vya utalii.

“Nitaendelea kuwapa msaada mtakaohitaji kwangu, ili muweze kufanya vizuri katika shindano lenu, kwani kupitia ninyi nchi yetu inaweza kutangazika ikiwa ni pamoja na kuvitangaza vivutio vyetu, pia ikiwa ni kuwapa changamoto,” alisema.

Aliongeza kuwa atakuwa akitoa mchango wake ili kuwezesha kuitangaza nchi iweze kujulikana kimataifa kwa kuendelea kuwapatia mahitaji mbalimbali washiriki wa mashindano hayo.

Warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo ambao ni pamoja na Flora Nicholaus(22), Edna Andrew(20),Taus Thomas(21),Sheimaa Ntetema(20),Janneth Samson(19), Sheila Said Baamary(23),Sauda Ramadhani(22), Ratifa Iddy(20), Rechal Isaya(19), Jamida Abdu(21) na Tickey Lighton(21).

Mratibu huyo aliongeza kuwa milango bado iko wazi kwa warembo wengine watakaohitaji kushiriki shindano hilo kujitokeza katika Ukumbi wa Da West Inn Park, Tabata ilipo kambi ya warembo hao.

Mbali na Aurora, wadhamini wengine ni pamoja na Kelken Fitness Center, Dage Saloon, Kiwanga Store & C0, Aucland Tours & Safari, The Grand Villa Hotel, Mashujaa Pub, Sayona Drinks Water, Moringa Oleifera, Image Smart, Valley Spring na Mh. Mussa Azan Zungu.
Wengine ni Papaa Msofe, VAM General Supply, Victor na Kariakoo, Mama Vanessa, makampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Babu Kubwa na Magazine & OK News Week, Kiu, San, Mh. Idd Azan.

 
Ismail Ally    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: rungu langu    Tuesday, October 20, 2009 19:48:51   
 
duh wengine dada zake semenya
 
 
Mtoa Maoni: kipara    Tuesday, October 20, 2009 20:18:51   
 
ingelikua kunatokea fani inajitokeza kwa mantiki ya kusaidia majanga mfano albino''mbagala''kipawa ikawa wanachangisha harambee ningelisapoti nyinyi wadanganyika mpo na starehe tuu vipii hamuandai mustakabali wa kizazii chenuu cha baadaee nyie mpo 2 kila siku marahaa 2 kweli sikio la kufa halisikii dawa wanawamalizeni aamkenii wadanganyika..........
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Tuesday, October 20, 2009 21:56:54   
 
miaka ya 70 tanganyika ilijulikana kwa madini yake ulimwenguni kote, Zenji kwa uuzaji wa karafuu ulimwenguni kote, hakukuwa na Miss wala Missa! leo tunaambiwa Miss ndio wanaitangaza Tz tokea lini, km si dili la wajanja kuona kua pana ulaji wa kutumia miili ya kina dada zao ili wanufaike ktk biashara zao!
"ke" amkeni, ingawa silaumu sana manake nchi yenyewe usipojichanganya utakufa na njaa na kupata wazimu usioutarajia kama yule alievamia jukwaa la FM.
utalii bila umeme???

 
 
Mtoa Maoni: ubuguvu    Tuesday, October 20, 2009 22:40:44   
 
wewe kipara na hizo fikra zako inaoneka wazi tz nchi yako tu lakini hukai BONGO maana hayo mawazo yako niya watu wapenda maedeleo na tz hakuna viongozi waopenda maendeleo,wengi hawataki nchi iendelee ndo maana hakuna Raisi anaefanikisha japo nusuya ahadi zake anapoingia madarakani anakua yupo pekeyake mtakamaedeleo wenzie wato wanapanga waibe vipi
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake