Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Kichaa Avamia Shoo ya FM Academia na Kuvua Nguo


Nwasuma si mchezo sema lilimuongezea ukichaa chizi huyu
Tuesday, October 20, 2009 1:32 AM
Kichaa mmoja mwanaume usiku wa jumapili alivamia shoo ya bendi ya FM Academia wakati wakitumbuiza katika ukumbi wa New Msasani Club jijini Dar es Salaam na kutinga jukwaani kabla ya kuanza kunengua huku akivua nguo zake na kubakia na shuka.
Kichaa mmoja usiku wa jumapili aliingia na kifurushi cha uchafu kwenye steji ambayo wapenzi wa FM Academia walijimwaga kulisakata ngwasuma na aliwaacha watu wengi wakipigwa na butwaa.

Walinzi wa ukumbi huo hawakujua chochote wakati watu waliupokuwa wakiukimbia ukumbi hasa sehemu ya steji maalumu kwaajili ya watu waliojitosa kulirudi Ngwasuma la FM Academia.

Kichaa huyo alionekana kuwa mjuzi zaidi wa kunengua baada ya kwenda sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo na alitia fora zaidi wakati kiongozi wa bendi hiyo alipopanda kuimba wimbo wa Henken .

Muda jinsi ulivyokuwa ukienda ndivyo ukichaa wake ulipozidi kupanda hadi ilipofikia hatua ya kuvua nguo zake na kuvaa shuka ambalo alikuwa amelificha katika kifurushi chake cha taka taka ambazo zilizagaa eneo la kuchezea.

Hata hivyo waimbaji FM Academia walikerwa na kichaa huyo ambaye vituko vyake vilianza kuwaudhi watu wengi na kupelekea mpiga ngoma wa bendi hiyo kuziacha ngoma zake na kwenda kumtoa nje ya ukumbi kichaa huyo.

Mwandishi wa Nifahamishe alimfuata nje kichaa huyo na kumuuliza jina lake na bila kusita alijibu anaitwa "Dokta Andrew" na anaishi katika maeneo ya Mikocheni B.

Kuingia kwa kichaa huyo kwenye ukumbi mpaka kufika kwenye steji kuu kulionyesha kuwa ukumbi huo hauna ulinzi wa kutosha kutokana na kwamba kichaa huyo alipita kwenye geti lenye mabaunsa kibao ambao walikomaa usiku mzima kuhakikisha watu wenye tiketi pekee ndio wanaoingia ukumbini.
  GONGA HAPA KWA PICHA ZAKE  

 
Na Kaimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: moms016    Tuesday, October 20, 2009 01:42:57   
 
Si kichaa wala nini, hii ni ile sera ya "maisha bora kwa kila mtanzania" huyu ni mmoja 2 kati ya mamilioni..
Vichaa ni hao mabaunsa waliokaa mlangoni, na kushindwa kumgundua muhusika na asiyehusika..kudadadeki!! Maisha tz tuachiliwe wenyewe roho za paka!!
Sahiba wangu NAUTIA K. nimekumiss mazee! upo?

 
 
Mtoa Maoni: edmundo    Tuesday, October 20, 2009 01:49:10   
 
hata mm mzee nakubaliana kabisa na mchangiaji huyo hapo juu..hapo hapana ukichaa mzee..ni hali halisi ya mtanzania alipofikishwa hapo.ww unadhani maisha hayo yalivyo hapo unafikiri huko mitaani wako wangapi kama hawa..hata bado? mara hii tutazalisha vichaa wengi tu..maana ndio kwanza mgao unakata mbuga..una depreciate uzalishaji kila siku zikenda...tunaambiwa sasa TANESCO inazalisha 90MGW badala ya 120MGW za zamani..tunakwenda nafikiri tukimaliza kikao cha bunge hapo tutakuwa tayari 6MGW.
 
 
Mtoa Maoni: Nautiakasi    Tuesday, October 20, 2009 02:37:21   
 
moms016 nipo mkuu, naomba ukumbi umechangamka siku hizi, watoa maoni ni wengi si haba, si kama enzi zile watoa maoni watu watatu tu Mark mushi, Ubuguvu na moms016. Tupopamoja twende kazi mkuu!
 
 
Mtoa Maoni: KING    Tuesday, October 20, 2009 10:06:55   
 
Kila siku ni vijimambo tu.....! Tushukuru huyu alivua nguo tu lkn kwa hakika wagonjwa wa akili ni hatari sana kuachwa uraiani wakijichanganya. Juzi tu mmoja kaua mtu A-town tukasema ni muhimu hawa wakawekwa panapo stahiri huko milembe, ili watibiwe manake kama 'zingecharuka' zaidi hapo ukumbini pata picha angeua wangapi huyu? Halafu wadau, chanzo cha magongwa ya akili ni jambo mtambuka sana na ugumu wa maisha ni moja tu kati ya thousands. Eee MOLA TUJAALIE WAJA WAKO AFYA NJEMA!
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Tuesday, October 20, 2009 16:30:27   
 
Nimefurahi kukusikia Sahiba wangu NAUTIA K. na mubarikiwe tu!
 
 
       Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi