Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Wasanii wa Maigizo Nchini Watakiwa Kwenda Shule


Steven Kanumba, miongoni mwa wasanii wa Bongo waliofanikiwa katika fani ya maigizo
Monday, October 19, 2009 11:07 PM
WASANII wa sanaa ya uigizaji nchini, wametakiwa kujiendeleza kielimu ili kuweza kuendesha kazi yao kwa ufanisi zaidi na kuepuka hali iliyojitokeza siku hizi ambapo sanaa ya maigizo imekuwa kimbilio la watu walioshindwa maisha.
Kauli hiyo imetolewa na mwalimu wa sanaa wa taasisi ya Youth Entertainment Campaign (YEC) Said Baraghash wakati taasisi hiyo ilipokuwa inazindua shindano la kusaka vipaji vya uigizaji la 'Ibua Filamu Star Tanzania' mapema wiki hii.

Baraghash alisema kuwa fani ya uigizaji kwa sasa imechukuliwa kama moja ya kimbilio la watu walioshindwa maisha, kitu ambacho ni hatari kwa maendeleo ya fani yenyewe.

Baraghash alisema kutokana na dhana hiyo washiriki walio wengi wamekuwa na mapungufu katika kutambua sheria na kanuni za fani hiyo hivyo kuwapa wakati mgumu kujenga uelewa wa wahusika.

Alisema katika mpango huo wa YEC, wanatarajia kuleta mapinduzi kwa kuwapa mafunzo ya saikolojia chipukizi watakaoshinda, kutokana na kile alichodai kuwa matatizo ya kisaikolojia ni tatizo kubwa kwa wasanii nchini.

"Kwa kweli tunakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwajengea uelewa wasanii wa fani hii hasa wale watakaopatikana katika shindano hili la Ibua Filamu Star Tanzania," alisema Baraghash.

Kwa upande wake Meneja Mipango wa YEC Adam Seleman maarufu kama (Swebe) alisema shindano hili litachangia kuibua vipaji vya vijana ambao wanaonekana kuwa na fani ya uigizaji.

Swebe alisema kwa kuanza mashindano hayo yatashirikisha mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam.

Meneja Mipango huyo alibainisha kuwa washiriki wanaohusika ni wenye umri kuanzia miaka 16 na kuendelea ambao hawajawahi kushiriki katika filamu yoyote.

Aidha alisema kupitia shindano hilo, wasanii watakaoonyesha viwango watashiriki katika filamu zitakazotolewa na kampuni hiyo ambazo zitasimama kuelezea mila na tamaduni za mtanzania.

Swebe alisema fomu za ushiriki zitatolewa katika mikoa husika ambapo siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo itakuwa Oktoba 30 mwaka huu na usahili utaanza Oktoba 31 Mjini Arusha.

 
Na Kaimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: moms016    Tuesday, October 20, 2009 01:48:59   
 
Kwanza: huyu Said Baraghash c ndo ktk wale watawala wa zenji hawa, sasa anataka nn?
Pili:hii fani ya kuigiza ss imetushinda kabsaa, ingawa tunajitahidi kwa mwendo wa jongoo, bora ileile michezo ya kina "pwagu na pwaguzi" (UBU kipindi hicho ni mtt sana)michezo ya redio zama za Marijani.
Alafu kuna kitu kinanishangaza sana, utakutia michezo ya kiswahili inapewa jina la kizungu sasa hii ndio kitu gani? kuwaiga Nigeria ama..?
Lkn c ya kukata tamaa iko siku tutatoka km Nigeria...

 
 
Mtoa Maoni: KING    Tuesday, October 20, 2009 10:15:25   
 
Hili kwa hakika ni la msingi sana....hakuna ufanisi mahali popote bila elimu bora ili kupata mwanga mzuri wa jambo husika. Wasanii wengi Tz wanafanya hii sanaa kimazoea na eti 'kipaji' tu. Hapana, wenzetu walioendelea sana huko duniani( au sio UBUGUVU?) ktk hii sanaa kama Hollywood na Bollywood wamepitia mafunzo maalum. Huamki tu eti ukapata tenda ya kushiriki movie hapo. NI WAKATI SASA ELIMU YA SANAA HUSIKA IKATILIWA MAANANI ILI KUONGEZA UBORA WA KAZI ZAO!
 
 
Mtoa Maoni: josephina msuya    Sunday, November 01, 2009 14:09:31   
 
mi sioni haja ya kuwaponda wasani kiivyo maana hiyo ni lugha ya watu hivi tumetawaliwa kiuchumi mpaka kiakili jamani hafikirii wenzentu wanajifunza salamu jambo na asante sana hata hicho cha kanumba kuna watu hawawezi kwani wamezaliwa huko ndo waongee bila kukosea watajifunza taratibu wataweza sio kuwasimanga bora huyo alie simama mbele ya watu akakose wanza kaosha kuitwa kwani wana jipelekaga wapo juu mta baki ng'eng'eng'e wenzenu wana songa mbele ambaye umeona hao hawajui sasa wewe kazana
 
 
Mtoa Maoni: jenny backpacke    Sunday, November 01, 2009 14:15:52   
 
ni kweli wasani wana takiwa kusoma na sio wasanii tu watu wote kwa ujumla wanatakiwa kula kitabu mfano mzuri kenya mpa muuza nyanya anapiga ngeli hivyo na watanzania tujitahidi nasio kupondana hayo ni mabo ya kishamba tuangalie mbele
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Si Uchawi ni Mazoezi tu..
> 'Wanamuziki wa Bongo Flava Tungeni Nyimbo zenye Ujumbe'
> 'Miss Kibonge' Apatikana Italia
> Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa
> Fella Ageukia Qaswida
> Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother
> Mrembo wa Temeke Apatikana
> Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?
> VIDEO - Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani
> VIDEO - Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube
> Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza
> 50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua
> Burudani Time - Nyama ya Bata
> Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
> Mrembo Mpya wa IFM Apatikana
> Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome
> Saleh Kupaza: ‘mchawi’ Aliyepewa Mwana kulea Twanga Pepeta
> 'Nipigie' ya AT Kuingia Sokoni
> Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao
> TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili
> Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...
> VIDEO - 'Tozi wa Mbagala' Kuingia Sokoni Mwezi Ujao
> Nyota wa Bongo Star Search Ajiunga na Mjomba Band
> Kapuya Aweka Uwaziri Pembeni na Kuanza Kupekecha
> Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi