Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Je Muziki wa Bongo Fleva Unakaribia Kupoteza Utamu Wake?


Joseph Haule 'Profesa Jay'
Tuesday, July 14, 2009 6:52 AM
KUANZIA mwanzoni mwa miaka ya 2000, ubongo wa vijana wengi wa Tanzania ulikuwa umejaa muziki wa Bongo Fleva. Unapowaona wamekaa vijana zaidi ya mmoja, basi mazungumzo yao yalikuwa ni juu ya muziki huo.Hata mavazi yalikuwa tofauti Suruali kubwa inayoacha makalio wazi, fulana kubwa na hereni kifuani.
KUANZIA mwanzoni mwa miaka ya 2000, ubongo wa wa vijana wengi wa Tanzania ulikuwa umejaa muziki wa Bongo Fleva. Unapowaona wamekaa vijana zaidi ya mmoja, basi mazungumzo yao yalikuwa ni juu ya muziki huo.

Hata mavazi yao, matamshi yao yalikuwa ni ya kibongo fleva. Suruali kubwa inayoacha makalio wazi, fulana kubwa na hereni kifuani. Hiyo ndiyo ilikuwa staili ya kukuonyesha kuwa wewe ni mwana BongoFleva.

Uumini wa vijana katika muziki huo, uliwafanya wengi wao kuamua kuwa waimbaji wa Bongo Fleva, ambapo wenyewe wanaita kushuka mistari.

Katika mazingira hayo kila kukicha kukawa kunaibuka wasanii wapya. Hawa wanajiandaa kuingia studio, wale wanaingia studio, yule anatoka studio na wengine wanaanza kusikika kwenye vyombo vya habari, televisheni na redio pamoja na kupamba kurasa za magazeti.

Hakuna kilichofanyika zaidi ya muziki. Baadhi yao walidiriki hata kuacha masomo ili ada za shule walizopewa na wazazi wao wakalipie studio.

Hali haikuwa hivyo kwa vijana pekee, kwani hata watu wazima nao ubongo wao ulitekwa na Bongo Fleva, hasa kutokana na masikio yao kulazimishwa na watangazaji wa redio na televisheni kusikiliza muziki huo. Kila kona ni Bongo Fleva.

Lakini wakati muziki huo unachukua chati, mwanamuziki mkongwe na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo 'Mjomba' alisema kuwa muziki huo ni sawa na Big G itafika kipindi utaanza kupoteza utamu.

Katika miaka ya hivi karibuni maneno hayo ya Gurumo kama yanaanza kutoa mwanga, kwani hali iliyouwa awali katika muziki huo inaanza kupotea.

Muziki huo umeanza kupoteza umaarufu wake kwenye vinywa vya vijana. Wengi waliokuwa na ndoto ya kuwa wasanii wa Bongo Fleva wameanza kurudi nyuma, huku wengi wao walioingia wanatoka.

Mavazi ya kibongofleva na swing (miondoko) ya kibongofleva yamepotea na wale ambao waliyatoa mawazo yao shuleni, sasa wameanza kuyarudisha.

Kana kwamba haitoshi leo hii ile kasi ya kusikika nyimbo mpya kila kukicha imepotea na hata zile zinazosikika ni chache zenye utamu. Nyingi zinakuwa ili mradi nyimbo.

Je kukosekana kwa matamasha na soko bovu la muziki nchini ndiyo sababu ya vijana kuanza kujitoa kwenye gemu la muziki huo?.

Joseph Haule 'Profesa Jay' na Ambwene Yesaya 'AY' wanakanusha hilo, na kusema kuwa woga na kutojiandaa kwa vijana ndiyo chanzo.

"Wengi wao walitaka kuingia kwenye gemu kwa kufuata pesa na umaarufu, lakini hawakuwa wamejiandaa kuwa katika safari hii watakutana na vikwazo vingi. Kubaki kwenye gemu kunahitaji ubishi na kujituma," alisema Profesa Jay.

"Kwa wale tuliojiandaa na tulioamua kufanya muziki kutokana na mapenzi bado tupo. Kwa mtu aliyejiandaa huwezi kuangalia soko la ndani pekee, lazima ujitafutie soko la nje," anasema AY.

Maneno ya wasanii hayo yana ukweli ndani yake, lakini pia yatumiwe kama dira kwa wanaotaka kuwa wana Bongo Fleva.

 
Na Kaimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: moms016    Tuesday, July 14, 2009 10:18:35   
 
mimi naungana na wanaoamini kuwa ulofa ndio chanzo cha kutoweka kwa utamu w muziki huu..
 
 
Mtoa Maoni: NOEL MICHAEL    Tuesday, July 14, 2009 11:02:14   
 
HUU MUZIKI WA BONGO FLEVA NI KWELI UKO KAMA UTAMU WA BAZOKA,MAANA NYIMBO ZILIZOPIGWA MIAKA YA 2000, TAYARI IKIPIGWA SASA INAKUWA KAMA ZILIPENDWA INAKUWA TOFAUTI NA NYIMBO ZA ENZI ZAKINA GURUMO AMBAZO MPAKA SASA BADO ZINAPENDEZA MASIKIONI,MAANA MUZIKI SI MASHAIRI TU ILA NI PAMOJA NA ALA ZILIZO PIGWA KIUFUNDI,KAMA WANA BONGO FLEVA WALIDHANI MUZIKI NI YALE MANENO TU,BASI WAMEKOSEA SANA. MUZIKI NI PAMOJA NA VYOMBO NDIO MAANA WATU WENGI TUNAPENDA MUZIKI WA KOFF OLOMIDE JAPO HATUJUI MAANA YAKE.
 
 
Mtoa Maoni: MGOGO    Tuesday, July 14, 2009 11:18:02   
 
NAKUBALIANA NA NOEL KWAMBA VIJANA WA BONGO FLEVA WAKITAKA MUZIKI WAO UDUMU LAZIMA WAJITUME,WAJIFUNZE ALA WAACHE KUINGIA STUDIO WAKIWA WANAMTEGEMEA MTU MMOJA,ILI MUZIKI UWE MTAMU HAUPASWI KUTEGEMEA MAWAZO YA MTU MMOJA HATA KAMA ANAJUA VYOMBO VYOTE KWA UFASAHA,MUZIKI MKAMILIFU NI KAMA MFANO WA MWILI WA MWANADAMU VIUNGO TOFAUTI UNAKAMILISHA MWILI HATA KWA VIUNGO VINAVYOONEKANA KANA KWAMBA HAVINA MAANA LAKINI VINA FAIDA YAKE,MUZIKI NI VIVYO NI MCHANGANYIKO WA WATU TOFAUTI WENYE MAWAZO TOFAUTI.
 
 
Mtoa Maoni: DAMIANI ARUSHA    Tuesday, July 14, 2009 11:28:48   
 
WANAOUPONDA MUZIKI WA BONGO FLEVA NI WAZEE AMBAO WANAPENDA MUZIKI WA ZAMANI SI KWA MAANA YA UZURI ILA UNAWAKUMBUSHA MAMBO YA ZAMANI,LAKINI SI KWAMBA UNA UZURI WOWOTE NA BONGO FLEVA HAIFI.
 
 
Mtoa Maoni: CHIBAGO    Tuesday, July 14, 2009 11:40:03   
 
BONGO FLEVA INAVUMA KWASASBABU RADIO NI NYINGI SASA HIVI NA WATANGAZAJI WENGI NI WAKIZAZI HICHO HICHO CHA BONGO FLEVA,RADIO HIZI ZINGEKUWEPO ZAMANI MUZIKI WA ZAMANI UNGEVUMA ZAIDI,REDIO YENYEWE ILIKUWA MOJA NA UPATIKANAJI WAKE ILIKUWAMARA NYINGINE HAIPATIKANI NA IKIPATIKANA INAKATISHA TAMAA KUISIKILIZA,KWA MUZIKI WA ZAMANI ULIKOSEKANA TU KUTANGAZWA KIKAMILIFU,NA HATA SASA KAMA UNGEPATA NAFASI YAKUPIGWA SANA NADHANI UNGEVUMA ZAIDI YA BONGO FLEVA.
 
 
       Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za burudani
> VIDEO - Wafungwa wa Filipino Watoa Video Mpya ya Michael Jackson
> VIDEO - Vunja Mbavu Kidogo..
> Nyota wa Marekani Atumia Viagra Kuinusuru Ndoa Yake
> Banana Zoro Aahidi Kuonyesha Makali Yake Mwaka Huu
> Bendi ya Sikinde Kufungua Matawi Kila Mkoa
> 'Rambo' Avunjika Shingo Wakati wa Kuigiza Filamu
> Beyonce na Jay-Z Wabadilisha Majina Yao
> Ndoa ya Wazazi Wake Beyonce Yavunjika
> VIDEO - Bibi wa Miaka 75 Awa Bingwa wa Kudansi
> Miss Burundi Awafunika Warembo toka Afrika Mashariki
> Mrisho Mpoto Aanzisha Bendi Yake inayoitwa 'Mjomba'
> Warembo wa East Africa Kuchuana kesho Uholanzi, Ray C kupagawisha
> Chokoraa Apigwa Stop Twanga Pepeta
> Blandina - Autosa Unesi Awe Msanii wa Maigizo
> Rihanna Akanusha Kumhonga Penzi Jay-Z
> 'Watanzania ni Wakarimu, Nitarudi Tena ' - Busta Rhymes
> Busta Rhymes Kuinogesha Fiesta Jioni Hii
> Unga Unawamaliza Wasanii wa Bongo Flava
> Miss Tanzania Akabidhiwa Mkoko Wake
> 'Natamani kuwa mwimbaji mahiri' - Aaliyah
> Ferre Gola kutua Bongo mwezi ujao
> Miss Tanzania Aanza Harakati Za Kutwaa Miss World
> Aurora Yajitosa Miss Utalii Ilala 2009
> Kichaa Avamia Shoo ya FM Academia na Kuvua Nguo
> Wasanii wa Maigizo Nchini Watakiwa Kwenda Shule

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Maadili yazidi kuporomoka Tan...
2 Meseji yazua utata kwa wanand...
3 Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mt...
4 Uingereza Kuzibania Viza Za W...
5 Skendo la Ununuzi wa Rada ya ...
6 Autoa Sadaka Ulimi Wake Ili A...
7 VIDEO - Drogba Aizamisha Arse...
8 Vitambulisho vya Taifa vitaan...
Photo Gallery
Photo Album

 Vituko vya Mapolisi Part 2
Random Photo

 Vijimambo vya Mr T
Habari Mpya Mpya
> Vitambulisho vya Taifa vitaanza kutolewa mwishoni mwa mwaka
> Maadili yazidi kuporomoka Tanzania
> Meseji yazua utata kwa wanandoa
> Skendo la Ununuzi wa Rada ya Tanzania, BAE Yapigwa Faini Dola Milioni 450
> Uingereza Kuzibania Viza Za Wanafunzi
> VIDEO - Drogba Aizamisha Arsenal
> Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mtoto
> Autoa Sadaka Ulimi Wake Ili Apate Mtoto
> Simba Na Yanga Zaenda Likizo Ligi Kuu
> Siku ya Wapendanao Patakuwa Hapatoshi Kwenye Mgahawa Huu