Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mama Mdogo Kuliko Wote duniani Kujifungua Mtoto wa Tatu


Stacey Herald anatarajia mtoto wa tatu ingawa madaktari wamemuonya maisha yake yako hatarini
Friday, November 13, 2009 6:46 AM
Mama mwenye umbile dogo kuliko wote duniani anatarajia kujifungua mtoto wa tatu ingawa madaktari wamemuonya kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na tumbo lake kuwa kubwa sana kuliko mwili wake kiasi cha kumfanya ashindwe hata kutembea.
Stacey Herald, ambaye ana urefu wa sentimeta 71 anatarajia kujifungua mtoto wa tatu ingawa madaktari wameendelea kumuonya kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na mimba aliyonayo.

Stacey alishayapuuza maoni ya madaktari mara mbili na kufanikiwa kujifungua watoto wawili ambao urefu wao wakati walipozaliwa ulikuwa ni zaidi ya nusu ya urefu wake.

Stacey mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Dry Ridge, Kentucky nchini Marekani anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Osteogenesis Imperfecta, ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu yenye kuvunjika kirahisi, mapafu dhoofu na ugonjwa huo umemsababishia asirefuke.

Stacey anaishi na mumewe Will mwenye urefu wa mita 1.75 na wanatarajia kupata mtoto wa tatu ndani ya wiki nne zijazo.

Kutokana na ukubwa wa tumbo lake la ujauzito, Stacey hawezi kufanya kazi yoyote ya nyumbani na humtegemea mumewe kufanya kazi hizo.

Kwa jinsi alivyo mfupi, mtoto wake atakayemzaa atakapofikisha umri wa mwaka mmoja atakuwa tayari ameishamzidi kwa urefu.

Pamoja na vikwazo vyote, wanandoa hao ambao walivalishana pingu za maisha mwaka 2004, wamesema wangependa kupata watoto zaidi.

Lakini madaktari wamemuonya Stacey kuwa mtoto aliye tumboni mwake anaendelea kukua na umbile lake litakuwa kubwa zaidi kuliko mwili wake mdogo na hivyo kupelekea viungo vyake vya ndani kupasuka na kupelekea kifo chake.

Hata hivyo Stacey amepania kuendelea na ujauzito wake kama mimba zake mbili zilizopita ambazo aliambiwa maneno kama hayo lakini aliyapuuza na kuzaa salama.

Mtoto wake wa kwanza Kateri alizaliwa mwaka 2006 akiwa na urefu nusu ya urefu wa mama yake kwa bahati mbaya alirithi ugonjwa wa mama yake kwahiyo naye pia hatarefuka atakuwa kama mama yake.

Stacey alipata mimba kwa mara nyingine mwaka uliofutia na alijifungua mtoto mwingine wa kike aliyepewa jina la Makaya.

Hivi sasa watoto wake wote wawili wana urefu zaidi ya mama yao.
  GONGA HAPA KWA PICHA ZA STACEY NA FAMILIA YAKE  

 
Source: News Agencies    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Ubuguvu    Friday, November 13, 2009 10:17:50   
 
Kwanza na mpongeza kwa kupata watoto na kua na moyo wakuta kuendea na kupata watoto zaidi na hasa kutokana na hali yake hapo baadae watamsaidia sana wakikua ni mamuzi ya kungwa mkuno na hasa ukingati huku majuu wanawake wengi wanatoa mimba na huko tz wanatupa watoto chooni lakini ushauri wa daktari ni muhimu kufaatwa kama mimc hii akijifungua salama bora ajizuie kupata mimba na nampongeza pia kwa mwanaume alitumia umahiri mkubwa mpaka akamfika ktk nanii au walipandika mbegu
 
 
Mtoa Maoni: ShaMusua    Friday, November 13, 2009 15:11:59   
 
Jamani, tuseme kweli wanaume hivi hata huruma hatuna??? inakuaje kumtendea mama kama huyu?? wanambaka au analilia????
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Friday, November 13, 2009 15:40:35   
 
"Je munaonaje manii muyatumbukizayo katika tumbo la uzazi? hivyo ninyi ndio munaoumba au sisi?" maneno ya kweli.. Ushauri wa daktari huwa kweli na haupingiki, lkn pamoja na yote kuna kudura isiyoingiliwa na kiumbe yyt. Kajifungua 2 za mwanzo na tunamuombea na ya 3 kwa kwenda mbele zitinge hewani.. inshalah. kwani c "ke" na anahitaji wtt?
UBUGUVU usishangae mkono hautafuti kinywa hata gizani unajua mdomo uko wapi!

 
 
Mtoa Maoni: mark.mushi    Friday, November 13, 2009 21:22:18   
 
duh e bwana hee ubuguvu umeongea point kweli,duh ata mimi nafikiri alimuweka juu ya meza adi kufikia down,sasa anazaa kwa operesheni au?
 
 
Mtoa Maoni: ShaMusua     Saturday, November 14, 2009 09:37:25   
 
hata kama ni njaa moms016 hekima itumike!!! kupitisha majamaa hali unajua hali ya mwenzako!!! mwenye mzigo hakutumia busara japo kwa dk 4

 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
More life style news and articles
> Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mtoto
> Mwanafunzi Aiuza Bikira Yake Kwa Dola 32,000
> Paka Anayedaiwa Kuwa na Uwezo wa Kunusa Kifo Kabla Hakijatokea
> Ana Miaka 13 Lakini Anaonekana Kama Bibi wa Miaka 50
> Uvaaji Wako wa Suruali Hudhihirisha Umri Wako
> Kibonge wa Dunia Apungua Kilo 127,Lakini Bado Anaongoza
> Kufanya Operesheni Ili Afanane na Supastaa wa Marekani
> Mtoto Aliyezaliwa Akiwa na Miguu Minne, Mikono Minne Aanza Shule
> Mwanaume Mwingine Apata Mimba, Kujifungua Mwezi Ujao
> Mume Mkware Ala Uroda na Mama Mkwe Wake
> VIDEO - Msichana wa India Anayevuja Damu Mara 50 Kwa Siku
> Mama Afanya Mapenzi Mara 200 na Mtoto wa Miaka 12
> Mchezaji Mweusi wa Marekani Abadili Rangi ya Ngozi Yake
> VIDEO - Tolu wa Dunia Alipokutana na Mtu Mfupi wa Dunia
> Makalio na Mapaja Makubwa ni Bora Kwa Afya
> Ana Mimba ya Miezi Mitano Lakini Bado Bikira
> Kwanini Watu Wengine Hata Wale Vipi Hawanenepi? Jibu la Kisayansi
> VIDEO - Mtoto wa Miaka 7 Mwenye Albamu Tatu za Muziki
> Miujiza ya Kijana Aliyefariki Yawapagawisha Wengi
> Mtoto wa Miaka 12 Amzalisha Mama Yake
> Ajali Yasababisha Awe na Hamu ya Mapenzi Wakati Wote
> Mtoto wa Mwaka Mmoja Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kuogelea
> Mtoto wa Miaka 6 Mwenye Uwezo wa Kuvuta Magari
> Mama Mdogo Kuliko Wote Duniani Ajifungua Mtoto wa Tatu
> Familia Inayoongea na Watu Waliofariki

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 Maadili yazidi kuporomoka Tan...
2 Meseji yazua utata kwa wanand...
3 Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mt...
4 Uingereza Kuzibania Viza Za W...
5 Skendo la Ununuzi wa Rada ya ...
6 Autoa Sadaka Ulimi Wake Ili A...
7 VIDEO - Drogba Aizamisha Arse...
8 Vitambulisho vya Taifa vitaan...
Photo Gallery
Photo Album

 Vituko vya Mapolisi Part 2
Random Photo

 Vijimambo vya Mr T
Habari Mpya Mpya
> Vitambulisho vya Taifa vitaanza kutolewa mwishoni mwa mwaka
> Maadili yazidi kuporomoka Tanzania
> Meseji yazua utata kwa wanandoa
> Skendo la Ununuzi wa Rada ya Tanzania, BAE Yapigwa Faini Dola Milioni 450
> Uingereza Kuzibania Viza Za Wanafunzi
> VIDEO - Drogba Aizamisha Arsenal
> Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mtoto
> Autoa Sadaka Ulimi Wake Ili Apate Mtoto
> Simba Na Yanga Zaenda Likizo Ligi Kuu
> Siku ya Wapendanao Patakuwa Hapatoshi Kwenye Mgahawa Huu