Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mashehe wapinga kampeni ya uzazi wa Mpango- Kilimanjaro
Advertisement


Thursday, July 02, 2009 10:24 AM
VIONGOZI wa dini ya kiislamu wakiwemo mashehe na maimamu wamepinga kampeni ya Taifa dhidi ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango nchini.
Hayo yalijulikana jana katika semina iliyowashirikisha viongozi hao wa dini iliyowataka watambue juu ya matumizi ya njia hizo Mkoani Kilimanjaro.

Kampeni hiyo ya Taifa ambayo ipo kwenye michakato ya kuwakutanisha viongozi wa dini mbalimbali nchini ili wapewe elimu ya njia hizo na wao wakawafikishie wananchi na kuwapa hamasa juu ya matumizi ya njia hizo.

Viongozi hao walipinga vikali juu ya kampeni hiyo na kusema kuwa hawatahamasisha jamii kwa kuwa njia hizo zinakwenda kinyume na maandiko ya dini hiyo.

Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya mashehe na viongozi wengine wa dini hiyo ya kiislamu wakiwemo na walimu wanawake wamesema kuwa kutokana na maandiko ya dini ya kiislamu kampeni hiyo ambayo wamepatiwa elimu wao hawataitekeleza kwa kuwa ni kinyume na maandiko ya dini.

Wamesema kuwa njia hizo kwanza ni kama ni kumkufuru mwenyezi mungu kwa kuwa yeye hakusema binadamu wazuie uzazi na kusema aliwataka wanadamu waje kuujaza ulimwengu na sio kuzuia kizazi.

Wamesema kuwa kampeni hiyo wanaipinga vikali na hawatawaambia waumini wao watumie njia hizo wao watawaelimsha waumini wao kulingana na maandiko yanavyosema.

Afisa Mipango zoezi la Mpango wa Uzazi wa Mpango Taifa, Bw. Safiel amesema kuwa, wanawakutanisha viongozi wa dini hao na wameonekana kama kutofahamu lengo la Taifa, na dhumuni la kuwakutanisha ni kutaka watambue njia hizo na waelimishe jamii juu ya njia hizo zinazoonekana wananchi walio wengi hawazitambui.

Na kusema kuwa sio kwamba wanawazuia wananchi wasizae bali kwa kudhibiti wimbi la watoto ambao hawapati huduma stahili kutoka kwa wazazi wao na vilevile kuelimisha jamii kuzaa kulingana na uwezo walio nao.

 
Na Chondoma Shabani, Dar es Salaam    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Ubuguvu    Thursday, July 02, 2009 14:53:51   
 
Bwana chondoma hukutuambia mafunzo yenyewe ni yapi ili tujue hao mashiekh walivmi jazba katika kukata kwao au wapo sawa kwasababu mimi mmoja katika mashiekh tena tumesomea shiekh
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Chadema yawasilisha pingamizi
> Wanafunzi waweweseka Tabata
> Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma yateketea
> Ramli ya Joseph ilisema hivi!
> 7 papohapo, wengine majeruhi ajalini- Mabibo
> Makahaba msipotoshe vazi hili!
> Sakata la kugombania maiti bado tata
> Mahakamani kwa kujipatia ngono kwa njia ya madawa ya kulevya
> Chadema yamuwekea pingamizi Kikwete
> Joseph aendelea na dozi
> Matatani kwa kujaribu kulawiti
> Hatma ya Muro Agosti 27
> JWTZ yatoa hofu wananchi
> Mwizi Auliwa Kwa Kuchomwa Moto Kichwa na Tumbo Lake
> Mwanamke akabiliwa na tuhuma za kujaribu kuua
> Joseph akimbizwa kwa mganga wa kienyeji
> Yu hatihati kufanya mtihani
> Maziko yatawaliwa na huzuni
> Aliyeshirikiana nae adaiwa yu mgonjwa kwa hofu
> Kikwete Aanguka Tena Jukwaani
> Sakata la paka mmoja afariki dunia
> Aliyetaka kuuza albino mzimamzima jela miaka 17

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 Siri ya Kimada Yafichuka
2 VIDEO - Mwanaume Anayemchezea...
3 Ajinyonga Baada ya Kunyimwa M...
4 Kampeni zachachamaa, wapinzan...
5 JK aendelea kutoa ahadi
6 Pingamizi la Chadema baada ya...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Jifotoe mama
Habari Mpya Mpya
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi
> Miaka 9 Jela Kwa Kuendesha Gari Huku Akiangalia Ngono
> VIDEO - Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1
> Kama Siku ya Kufa Haijafika...